>>JUMAPILI MEI 19: WBA v MAN UNITED, ENZI YA SIR ALEX KWISHA!
>>WANAHABARI WAMTANIA NA KEKI ‘MASHINE KUKAUSHIA NYWELE!’’
JUMAPILI,
MEI 19, ni Siku ya Mwisho ya Msimu wa BPL, Barclays Premier League, wa
2012/13 na Siku hiyo ndio Mechi ya 1500 kwa Sir Alex Ferguson akiwa
Meneja wa Manchester United na ndio mwisho wa enzi yake kwa vile
anastaafu.
Akiwa ametwaa Makombe 38 ndani ya Miaka
26 aliyodumu Man United, Sir Alex Ferguson, Miaka 71, amenena: “Ni Mechi
1500…Gemu yangu ya mwisho… inashangaza! Nataka kushinda hii kupita ile
ya Wiki iliyopita!”
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
SIR ALEX: MAKOMBE AKIWA MAN UNITED
LIGI KUU: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999, 2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013
FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
UEFA CHAMPIONZ LIGI: 1999, 2008
UEFA KOMBE LA WASHINDI: 1991
FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
UEFA SUPER CUP: 1992
INTER-CONTINENTAL CUP: 1999
FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Jumapili iliyopita Sir Alex Ferguson
aliagwa kwa shangwe walipocheza Mechi na Swansea City Uwanjani Old
Trafford, ikiwa ni Mechi yake ya mwisho Uwanjani hapo, na kushinda Bao
2-1 na Jumatatu Timu nzima ya Man United ilitembeza Kombe la Ubingwa wa
BPL kwenye Mitaa ya Manchester na kusindikizwa na Maelfu ya Washabiki
hadi katikati ya Jiji, eneo la Albert Square, walipopokewa na Maelfu ya
Umati.
Mwenyewe Ferguson amekiri kuwa mapokezi
ya Wiki iliyopita yalishinda yale ya Mwaka 1999 walipopita Mitaani baada
ya kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa England, FA CUP na UCL, UEFA
CHAMPIONZ LIGI, na kuweka Historia ya kuwa Klabu ya kwanza na pekee
Uingereza kufanya hilo.
Leo, kwenye Mkutano na Wanahabari kwenye
Kambi ya Mazoezi ya Man United huko Carrington ambao ni kawaida ya kila
Ijumaa kabla Mechi za Wikiendi, Wanahabari walimpa Sir Alex Ferguson
zawadi ya Keki yenye umbo la Mashine ya Kukaushia Nywele ukiwa ni mzaha
kuhusu imani ya kwamba Meneja huyo huwapa kibano Wachezaji wake
wasipofanya vizuri na kuwafanya wajisikie vichwa vyao moto mithili ya
kupitishiwa Mashine hiyo ya Kukaushia Nywele.
Akijibu kwa mzaha, Ferguson alisema:
“Inastahili! Kuna wakati sikukubaliana nanyi na kile kilichoandikwa na
kuna wakati mliandika vitu vizuri tu na nilividharau. Lakini Siku zote
sikuweka kinyongo wala kisasi. Hiyo si staili yangu!”
Ferguson pia alithibitisha kuwa Kipa
Anders Lindegaard atakaa Golini Mechi na WBA na Masentahafu watakuwa
Jonny Evans na Phil Jones huku Nemanja Vidic na Rio Ferdinand wakiwa
Benchi akisisitiza sasa ni zama za Vijana.
+++++++++++++++++++++++
BPL: RATIBA-MECHI ZA MWISHO MSIMU HUU
Jumapili 19 Mei
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Everton
Liverpool v QPR
Man City v Norwich
Newcastle v Arsenal
Southampton v Stoke
Swansea v Fulham
Tottenham v Sunderland
West Brom v Man United
West Ham v Reading
Wigan v Aston Villa
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
**MAN UNITED BINGWA
NA
|
TIMU
|
P
|
GD
|
PTS
|
1
|
Man United
|
37
|
43
|
88
|
2
|
Man City
|
37
|
33
|
78
|
3
|
Chelsea
|
37
|
35
|
72
|
4
|
Arsenal
|
37
|
34
|
70
|
5
|
Tottenham
|
37
|
19
|
69
|
6
|
Everton
|
37
|
16
|
63
|
7
|
Liverpool
|
37
|
27
|
58
|
8
|
West Brom
|
37
|
-4
|
48
|
9
|
Swansea
|
37
|
-1
|
46
|
10
|
West Ham
|
37
|
-10
|
43
|
11
|
Stoke
|
37
|
-11
|
41
|
12
|
Norwich
|
37
|
-18
|
41
|
13
|
Newcastle
|
37
|
-22
|
41
|
14
|
Southampton
|
37
|
-11
|
40
|
15
|
Fulham
|
37
|
-13
|
40
|
16
|
Aston Villa
|
37
|
-22
|
40
|
17
|
Sunderland
|
37
|
-12
|
39
|
18
|
Wigan *
|
37
|
-26
|
35
|
19
|
Reading *
|
37
|
-28
|
28
|
20
|
QPR *
|
37
|
-29
|
25
|
*ZIMESHUKA DARAJA
++++++++++++++++++++++++++++++++++
NI LEJENDARI SIR ALEX FERGUSON
ASANTE SANA NA MOLA AKUBARIKI!!
++NA Storming Fo
Ni mpenzi wa Michezo na maishani mwangu, tangu utoto wangu wako Mashujaa wa Kimichezo, niliowapenda.
Lakini, kimaisha, daima ndani ya
moyo wangu ukiondoa Wazazi wangu na Ndugu zangu wa damu, Shujaa mkubwa
kwangu na wa pekee ni MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE!!
YEYE, Siku zote husema, HE WAS THE BEST LEADER GOD EVER GAVE A POOR NATION!
Kwenye michezo ni Muhammad Ali.
Wakati Cassius Clay akiibuka
ndio enzi hizo hizo England inachukua Ubingwa wa Dunia wakiwa na
Wachezaji wa Manchester United Nobby Stiles na Bobby Charlton.
Hiyo ilikuwa Mwaka 1966 na ndio kipindi hicho hicho Cassius Clay akawa Muhammad Ali na Lejendari akazaliwa.
Bobby Charlton, sasa ni SIR
BOBBY CHARLTON, mara baada ya yeye na Kaka yake Jackie Charlton aliekuwa
akiichezea Leeds United, kuisaidia England kutwaa Kombe la Dunia Mwaka
1966 Uwanjani Wembley, aliandika Kitabu: FORWARD FOR ENGLAND, Kitabu
kilichozungumzia maisha yake ikiwemo kunusurika Ajali ya Ndege iliyoua
nusu ya Timu ya Manchester United Uwanja wa Ndege wa Munich Mwaka 1958.
Kitabu hicho nilipewa Miaka hiyo
hiyo kilipotoka na Kaka yangu, Baba mmoja Mama mmoja ‘aliesaliti’ Ukoo
wetu kwa kuichezea Sunderland, sasa ndio hii Simba, wakati Ukoo wetu ni
Yanga damu.
Mie baadae nilihamia Pan Africans lakini hadi hii leo Simba, si Yanga, ni ‘adui’ kwangu!
Kitabu hicho, FORWARD FOR ENGLAND, kilinifanya niipende Manchester United tangu wakati huo hadi hii leo.
Niliifuatilia sana Man United
kupitia Magazeti na BBC, ikishuka Daraja na kupanda tena, hadi Novemba
1986 alipotua Mtoto wa Kuli wa Poti ya Govan, Alex Ferguson, kuleta
Mapinduzi.
Kuanzia hapo hadi sasa, wanavyosema Wahenga ni Historia!
Manchester United iliibuka na
kusambaratisha Timu zote England, hasa Liverpool waliokuwa Wababe,
kutetemesha Ulaya na Dunia na kukubalika kuanzia huko Manchester, kila
kona ya Dunia hadi kule kwetu Samvula Chole.
Yote ni kazi ya Alex Ferguson, sasa ni SIR Alex Ferguson!
Upo wakati nilikufurahia sana,
upo wakati ulinichukiza, hasa staili yako ya kubadilisha Wachezaji kila
Mechi kupindukia, kitu ambacho wakati mwingine kilileta madhara, lakini
kila wakati ulidhihirisha wewe ni MSHINDI!
UNASTAHILI HESHIMA, SIR ALEX FERGUSON!
NAKUTAKIA KILA LA HERI MAISHA YAKO YA BAADAE!
ASANTE SANA NA MOLA AKUBARIKI!!
BILA KUPINGWA,
WEWE NI LEJENDARI!!