Friday, May 17, 2013

DABI YA KARIAKOO: SHANGWE JANGWANI AU MSIMBAZI???


>>MGAMBO, POLISI, TOTO, 2 ZIPI KUIFUATA LYON CHINI??
DABI_YA_KARIAKOOVPL, LIGI KUU VODACOM, inafika tamati Jumamosi Mei 18 wakati tayari Bingwa ni Yanga, Mshindi wa Pili ni Azam FC na kilichobaki ni Timu zipi mbili zitaungana na African Lyon kucheza FDL Msimu ujao lakini bado BIGI MECHI ni ile ile DABI ya KARIAKOO kati ya Yanga na Simba.
Siku zote ni Bigi Mechi Yanga na Simba lakini safari hii  ‘kachumbari’ hamna maana tayari Yanga ni Bingwa na Nafasi ya Pili imechukuliwa na Azam FC na Simba watabaki Nafasi ya Tatu tu, na hivyo kutocheza Klabu Afrika Msimu ujao, lakini Siku zote Mechi hii ni ya ushindani uliojaa kila majigambo, sifa na hekaheka kila Kona ya Dar es Salaam na Nchi nzima.
Hii ndio DABI ya KARIAKOO, Mechi tangu zama za zamani ina vituko, shamrashamra na kila aina ya vioja.
Na ndio maana Timu zote, Yanga na Simba, zilipiga Kambi nje ya Dar es Salaam huko Visiwani Unguja, kwa Yanga, chini ya Kocha wao toka Uholanzi Ernie Brandts, kuwa Pemba, na Simba, chini ya Mfaransa, Patrick Liewig, kutua huko Zanzibar.
Hii ni mara ya Pili Timu hizi kukutana Msimu huu kweye VPL na mara ya kwanza matokeo yalikuwa Bao 1-1 hapo Oktoba 3, 2012.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUMBUKUMBU TU-3 OKTOBA 2012:
YANGA 1 SIMBA 1
Simba ndio walitangulia kupata bao Dakika ya 4 tu ya mchezo kwa bao la Amri Kiemba baada ya kupokea pande zuri toka kwa Mwinyi Kazimoto.
Hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Yanga walisawazisha bao kwa Penati katika Dakika ya 66 baada ya Ngalema kuunawa mpira na Penati hiyo kufungwa na Saidi Bahanuzi.
Baada ya hapo Yanga walipata pigo baada ya Chipukizi wao Simon Msuva kupewa Kadi Nyekundu kwa kumpiga Juma Nyosso.
Matokeo haya yameifanya Simba iwe na Pointi 13 kwa Mechi 5 na Yanga kuwa na Pointi 8 kwa idadi hiyo hiyo ya Mechi.
VIKOSI:
SIMBA: Juma Kaseja, Nassor Chollo, Paul Ngalema, Juma Nyosso, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Edward Christopher, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Mrisho Ngassa.
Akiba: Wilbert Mweta, Komabil Keta, Paschal Ochieng, Kiggi Makassy, Salum Kinje, Daniel Akuffo, Abdallah Juma na Ramadhan Chombo ‘Redondo’
YANGA: Yaw Berko, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Cannavaro, Kevin Yondan, Athumani Iddi, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi na Hamisi Kiiza.
Akiba: Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Godfrey Taita, Stafano Mwasyika, Job Ibrahim, Frank Domayo, Nizar Khalfan, Shamte Ally, Idrisa Rajab na Jerry Tegete.
Refa: Mathew Akrama
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi Mei 18
Toto Africans Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs African Lyon
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
TZ Prisons Vs Kagera Sugar
Simba SC Vs Yanga SC
JKT Oljoro Vs Azam FC
Polisi Moro Vs Coastal Union
MSIMAMO:
***YANGA+++BINGWA
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
YANGA
25
17
6
2
45
14
31
57
2
AZAM FC
25
15
6
4
45
20
25
51
3
SIMBA SC
25
12
9
4
38
23
15
45
4
KAGERA SUGAR
25
11
8
6
26
19
7
41
5
MTIBWA SUGAR
25
10
9
6
29
24
5
39
6
COASTAL UNION
25
8
11
6
25
23
2
35
7
RUVU SHOOTING
25
8
8
9
22
24
-2
32
8
JKT OLJORO
25
7
8
10
21
26
-5
29
9
TANZANIA PRISONS
25
7
8
10
16
22
-6
29
10
JKT RUVU
25
7
5
13
21
38
-17
26
11
MGAMBO SHOOTING
25
7
4
14
16
27
-11
25
12
POLISI MOROGORO
25
4
10
11
13
23
-10
22
13
TOTO AFRICAN
25
4
10
11
21
33
-12
22
14
AFRICAN LYON
25
5
4
16
16
38
-22
19
***AFRICAN LYON IMESHUKA DARAJA
WAOWAHI KUWA MABINGWA:
1965 Sunderland (Sasa inaitwa Simba SC)
1966 Sunderland
1967 Cosmopolitan
1968 Young Africans
1969 Young Africans
1970 Young Africans
1971 Young Africans
1972 Young Africans
1973 Simba SC
1974 Young Africans
1975 Mseto SC
1976 Simba SC
1977 Simba SC
1978 Simba SC
1979 Simba SC
1980 Simba SC
1981 Young Africans
1982 Pan Africans
1983 Young Africans
1984 Simba SC
1985 Young Africans
1986 Tukuyu Stars
1987 Young Africans
1988 Coastal Union
1989 Young Africans
1990 Simba SC
1991 Young Africans
1992 Young Africans
1993 Young Africans
1994 Simba SC
1995 Simba SC
1996 Young Africans
1997 Young Africans
1998 Young Africans
1999 Mtibwa Sugar
2000 Mtibwa Sugar
2001 Simba SC
2002 Young Africans
2003 Simba SC
2004 Simba SC
2005 Young Africans
2006 Young Africans
2007 Simba SC
2007/08 Young Africans
2008/09 Young Africans
2009/2010 Simba SC
2010/2011 Young Africans
2011/2012 Simba SC
2012/2013 Young Africans

GEMU 1500: NI MWISHO KWA LEJENDARI SIR ALEX!


>>JUMAPILI MEI 19: WBA v MAN UNITED, ENZI YA SIR ALEX KWISHA!
>>WANAHABARI WAMTANIA NA KEKI ‘MASHINE KUKAUSHIA NYWELE!’’
FERGUSON_-MIKONO_JUUJUMAPILI, MEI 19, ni Siku ya Mwisho ya Msimu wa BPL, Barclays Premier League, wa 2012/13 na Siku hiyo ndio Mechi ya 1500 kwa Sir Alex Ferguson akiwa Meneja wa Manchester United na ndio mwisho wa enzi yake kwa vile anastaafu.
Akiwa ametwaa Makombe 38 ndani ya Miaka 26 aliyodumu Man United, Sir Alex Ferguson, Miaka 71, amenena: “Ni Mechi 1500…Gemu yangu ya mwisho… inashangaza! Nataka kushinda hii kupita ile ya Wiki iliyopita!”
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
SIR ALEX: MAKOMBE AKIWA MAN UNITED
LIGI KUU: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999, 2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013
FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
UEFA CHAMPIONZ LIGI: 1999, 2008
UEFA KOMBE LA WASHINDI: 1991
FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
UEFA SUPER CUP: 1992
INTER-CONTINENTAL CUP: 1999
FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Jumapili iliyopita Sir Alex Ferguson aliagwa kwa shangwe walipocheza Mechi na Swansea City Uwanjani Old Trafford, ikiwa ni Mechi yake ya mwisho Uwanjani hapo, na kushinda Bao 2-1 na Jumatatu Timu nzima ya Man United ilitembeza Kombe la Ubingwa wa BPL kwenye Mitaa ya Manchester na kusindikizwa na Maelfu ya Washabiki hadi katikati ya Jiji, eneo la Albert Square, walipopokewa na Maelfu ya Umati.
Mwenyewe Ferguson amekiri kuwa mapokezi ya Wiki iliyopita yalishinda yale ya Mwaka 1999 walipopita Mitaani baada ya kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa England, FA CUP na UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, na kuweka Historia ya kuwa Klabu ya kwanza na pekee Uingereza kufanya hilo.
Leo, kwenye Mkutano na Wanahabari kwenye Kambi ya Mazoezi ya Man United huko Carrington ambao ni kawaida ya kila Ijumaa kabla Mechi za Wikiendi, Wanahabari walimpa Sir Alex Ferguson zawadi ya Keki yenye umbo la Mashine ya Kukaushia Nywele ukiwa ni mzaha kuhusu imani ya kwamba Meneja huyo huwapa kibano Wachezaji wake wasipofanya vizuri na kuwafanya wajisikie vichwa vyao moto mithili ya kupitishiwa Mashine hiyo ya Kukaushia Nywele.
Akijibu kwa mzaha, Ferguson alisema: “Inastahili! Kuna wakati sikukubaliana nanyi na kile kilichoandikwa na kuna wakati mliandika vitu vizuri tu na nilividharau. Lakini Siku zote sikuweka kinyongo wala kisasi. Hiyo si staili yangu!”
Ferguson pia alithibitisha kuwa Kipa Anders Lindegaard atakaa Golini Mechi na WBA na Masentahafu watakuwa Jonny Evans na Phil Jones huku Nemanja Vidic na Rio Ferdinand wakiwa Benchi akisisitiza sasa ni zama za Vijana.
+++++++++++++++++++++++
BPL: RATIBA-MECHI ZA MWISHO MSIMU HUU
Jumapili 19 Mei
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Everton
Liverpool v QPR
Man City v Norwich
Newcastle v Arsenal
Southampton v Stoke
Swansea v Fulham
Tottenham v Sunderland
West Brom v Man United
West Ham v Reading
Wigan v Aston Villa
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
**MAN UNITED BINGWA
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Man United
37
43
88
2
Man City
37
33
78
3
Chelsea
37
35
72
4
Arsenal
37
34
70
5
Tottenham
37
19
69
6
Everton
37
16
63
7
Liverpool
37
27
58
8
West Brom
37
-4
48
9
Swansea
37
-1
46
10
West Ham
37
-10
43
11
Stoke
37
-11
41
12
Norwich
37
-18
41
13
Newcastle
37
-22
41
14
Southampton
37
-11
40
15
Fulham
37
-13
40
16
Aston Villa
37
-22
40
17
Sunderland
37
-12
39
18
Wigan *
37
-26
35
19
Reading *
37
-28
28
20
QPR *
37
-29
25
*ZIMESHUKA DARAJA
++++++++++++++++++++++++++++++++++
NI LEJENDARI SIR ALEX FERGUSON
ASANTE SANA NA MOLA AKUBARIKI!!
++NA Storming Fo
Ni mpenzi wa Michezo na maishani mwangu, tangu utoto wangu wako Mashujaa wa Kimichezo, niliowapenda.
Lakini, kimaisha, daima ndani ya moyo wangu ukiondoa Wazazi wangu na Ndugu zangu wa damu, Shujaa mkubwa kwangu na wa pekee ni MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE!!
YEYE, Siku zote husema, HE WAS THE BEST LEADER GOD EVER GAVE A POOR NATION!
Kwenye michezo ni Muhammad Ali.
Wakati Cassius Clay akiibuka ndio enzi hizo hizo England inachukua Ubingwa wa Dunia wakiwa na Wachezaji wa Manchester United Nobby Stiles na Bobby Charlton.
Hiyo ilikuwa Mwaka 1966 na ndio kipindi hicho hicho Cassius Clay akawa Muhammad Ali na Lejendari akazaliwa.
Bobby Charlton, sasa ni SIR BOBBY CHARLTON, mara baada ya yeye na Kaka yake Jackie Charlton aliekuwa akiichezea Leeds United, kuisaidia England kutwaa Kombe la Dunia Mwaka 1966 Uwanjani Wembley, aliandika Kitabu: FORWARD FOR ENGLAND, Kitabu kilichozungumzia maisha yake ikiwemo kunusurika Ajali ya Ndege iliyoua nusu ya Timu ya Manchester United Uwanja wa Ndege wa Munich Mwaka 1958.
Kitabu hicho nilipewa Miaka hiyo hiyo kilipotoka na Kaka yangu, Baba mmoja Mama mmoja ‘aliesaliti’ Ukoo wetu kwa kuichezea Sunderland, sasa ndio hii Simba, wakati Ukoo wetu ni Yanga damu.
Mie baadae nilihamia Pan Africans lakini hadi hii leo Simba, si Yanga, ni ‘adui’ kwangu!
Kitabu hicho, FORWARD FOR ENGLAND, kilinifanya niipende Manchester United tangu wakati huo hadi hii leo.
Niliifuatilia sana Man United kupitia Magazeti na BBC, ikishuka Daraja na kupanda tena, hadi Novemba 1986 alipotua Mtoto wa Kuli wa Poti ya Govan, Alex Ferguson, kuleta Mapinduzi.
Kuanzia hapo hadi sasa, wanavyosema Wahenga ni Historia!
Manchester United iliibuka na kusambaratisha Timu zote England, hasa Liverpool waliokuwa Wababe, kutetemesha Ulaya na Dunia na kukubalika kuanzia huko Manchester, kila kona ya Dunia hadi kule kwetu Samvula Chole.
Yote ni kazi ya Alex Ferguson, sasa ni SIR Alex Ferguson!
Upo wakati nilikufurahia sana, upo wakati ulinichukiza, hasa staili yako ya kubadilisha Wachezaji kila Mechi kupindukia, kitu ambacho wakati mwingine kilileta madhara, lakini kila wakati ulidhihirisha wewe ni MSHINDI!
UNASTAHILI HESHIMA, SIR ALEX FERGUSON!
NAKUTAKIA KILA LA HERI MAISHA YAKO YA BAADAE!
ASANTE SANA NA MOLA AKUBARIKI!!
BILA KUPINGWA,
WEWE NI LEJENDARI!!

ZIMECHEZWA SIMBA NA YANGA ZOTE, HAIJAWAHI KUTOKEA TAMU KAMA HII


Na mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 17, 2013, SAA 12:00 ASUBUHI
NYASI za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zinatarajiwa kuwaka moto kesho, Jumamosi (Mei 18, 2013) kwa mpambano wa watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga. Huo utakuwa mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wakiwa tayari wamewavua ubingwa wapinzani wao wa jadi, Simba SC. BIN ZUBEIRY inaendelea kukuletea mfululizo wa makala za kuelekea pambano hilo linalobeba picha halisi ya soka ya Tanzania na leo tunahamia kwenye mchezo mzuri zaidi kuwahi kutokea kihistoria baina ya michezo iliyowahi kuwakutanisha wapinzani hao wa jadi. Endelea.
Moja ya mechi za Simba na Yanga hivi karibuni, Nsa Job akipiga tik tak mbele ya Juma Nyosso

KUNA mechi Yanga iliifunga Simba 5-0. Kuna mechi Simba iliifunga Yanga 6-0 na ile ya mwaka jana ya 5-0. Lakini kwa mujibu wa wazoefu wa kushuhudia mechi baina ya miamba hiyo, haujawahi kutokea mchezo mkali wa Simba na Yanga kama ule wa Agosti 10, mwaka 1974.
Huo ulifanyika katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza ukiwa ni mchezo wa Fainali ya Klabu Bingwa ya Taifa na Yanga wakatoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 baada ya dakika 120.
Mapema dakika ya 16, Adam Sabu (sasa marehemu) aliyekuwa akiitwa Gerd Muller akifananishwa na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani, aliifungia Simba bao la kuongoza ambalo lilidumu hadi kipindi cha pili.
Wakati baadhi ya watu wanaanza kuinuka kwenye Uwanja wa Nyamagana, wakiamini Simba SC imetetea ubingwa wake kwa bao pekee la Sabu, mshambuliaji aliyekuwa ana misuli ya nguvu ya kufumua mashuti makali, Gibson Sembuli (sasa marehemu pia) akaisawazishia Yanga, zikiwa zimebaki dakika tatu mchezo kumalizika, yaani dakika ya 87.
Kwa sababu huyo, mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza na katika dakika ya saba ya muda huo, mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika ardhi ya Tanzania daima, Sunday Manara ‘Computer’ akaifungia Yanga bao la pili na la ushindi dakika ya 97.
Yanga ikarejesha ubingwa wake, kwa ushindi wa 2-1 katika pambano la kwanza kabisa baina ya watani wa jadi kufanyika nje ya ardhi ya Dar es Salaam.
Hapa ni Nyamagana Agosti 10, 1974 Kipa wa Simba Athumani Mambosasa akiwa amedaka mpira wa juu mbele ya Kitwana Manara wa Yanga, huku akilindwa na beki wake Jumanne Masimenti kulia. Haijatokea mechi tamu ya watani kama hii hadi sasa. 

KWA NINI PAMBANO BORA ZAIDI LA WATANI?
KATIKA kujiandaa na msimu wa 1974, Simba SC walifanya ziara ya mafunzo nchini Poland, wakati Yanga SC nao walikwenda Romania.
Lakini pia, kikosi cha Simba SC ni ambacho kilitwaa ubingwa msimu uliotangulia mwaka 1973 na pia ndicho kilitwaa Kombe la Afrika Mashariki na Kati mwaka 1974 pamoja na kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka huo, wakatolewa na Mehallal El Kubra ya Misri, wakitoka kuwatoa Hearts Of Oak ya Ghana.
Kwa Yanga, kikosi chao kilikuwa kinaundwa na nyota wengi walioifikisha timu hiyo Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika mara mbili mfululizo, 1969 na 1970 mara zote ikitolewa na Asante Kotoko ya Ghana kwa mbinde- hivyo ukichanganya na mazoezi ya Poland na Romania, timu hizo zilikuwa moto.  
Timu hizo ziliporejea nchini, zikakutana katika kituo cha mwaka huo cha Klabu Bingwa ya Taifa, mjini Mwanza enzi hizo ligi ikichezwa katika mtindo kama wa Kombe la Taifa, kunakuwa na kituo na makundi mawili na baadaye washindi wa makundi wanakutana katika fainali.
Simba na Yanga ziliongoza makundi yao na zikakutana katika fainali mjini Mwanza, mchezo ambao ulikuwa gumzo mno- mamia walisafiri kutoka mikoa mbalimbali kuelekea mjini Mwanza, wakiwemo wakazi wa Dar es Salaam. Mwanza ilifurika na Nyamagana hapakutosha.
Wakati huo, Simba SC kambi yao ilikuwa katikati ya Jiji la Mwanza tu, hoteli moja maarufu enzi hizo, Sukumaland wakati Yanga walikuwa wanaweka kambi yao Butimba.
Ikumbukwe katika mashindano ya mwaka huo, Simba SC ilimkosa kiungo wake mahiri, Khalid Abeid ambaye alikuwa majeruhi, lakini kwa mchecheto wa mechi hiyo, walitaka kumlazimisha kucheza, ila ikashindikana kwa sababu hakuwa fiti.
Ilikuwa mechi kali na ya ushindani na siku hiyo, mshambuliaji wa Simba SC, Saad Ali alizirai uwanjani baada ya kupigwa na mpira uliopigwa na Sembuli, akakimbizwa hospitali, ambako ilielezwa hakupata fahamu hadi siku ya pili. Mbaya zaidi, usiku ilivumishwa Saad amefariki dunia, lakini alipona.
Kuna uvumi fulani, eti sehemu ambayo aliangukia Saad paliota kichuguu ambacho miaka nenda, rudi hakipotei Nyamagana. 
Aidha, mshambuliaji mwingine wa Simba SC, Willy Mwaijibe naye aligongana na kipa wa Yanga SC, Elias Michael ‘Nyoka Mweusi’ na wakaumia wote na kutoka nje. Nafasi ya Mwaijibe aliingia Adam Sekulu na nafasi ya Michael aliingia Muhiddin Fadhil.
Walioshuhudia wanasema soka ilichezwa Nyamagana Agosti 10 ya mwaka 1974, enzi hizo Simba na Yanga, Simba na Yanga kweli kuanzia wachezaji, viongozi hadi wapenzi. Hadi tunaingia katika milenia mpya, bado haijatokea mechi nyingine ya kufananishwa na hiyo.
Katika mchezo huo, vikosi vilikuwa; Yanga SC; Elias Michael/Muhiddin Fadhil, Suleiman Sanga, Boy Wickens, Hassan Gobbos, Omar Kapera, Abdulrahman Juma, Leonard Chitete, Sunday Manara, Gibson Sembuli, Kitwana Manara na Maulid Dilunga.  
Simba SC; Athumani Mambosasa, Shaaban Baraza, Mohamed Kajole, Jumanne Masimenti, Omar Chogo, Omar Gumbo, Wily Mwaijibe/Adam Sekulu, Haidari Abeid ‘Muchacho’, Adam Sabu, Abdallah Kibadeni na Saad Ally/Abbas Dilunga.
Simba SC walikwenda Oman kabla ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Yanga walikwenda Uturuki- huwezi kuona dalili za kesho kupatikana Simba na Yanga bora kuliko ile ya Agosti 10, 1974. Tuheshimiane jamani.
 BY.BIN ZUBEIR

BREAKING NEWSSSSSSSSS.POLISI MSTAAFU AMCHARANGA MWANAE WA MIAKA 4 KWA MAPANGA .SAMAHANI MSOMAJI KWA BAADHI YA PICHA UTAKAZOZIONA.



ASKARI POLISI MSTAAFU SAMSON BWIRE AKIWA AMEFIKISHWA HOSPITALINI MDA MCHACHE BAADA YA KURUKA KUTOKA KWENYE GARI AKIJARIBU KUKIMBIA.
KAHAMA.
Mkazi wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54), anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumcharanga mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa kimapenzi.
Tukio hilo limetokea leo jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake Happiness Elius (28)  huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.
Kwa mujibu wa majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda walimkuta Bwire akichoma nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na kuanza kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango.
Imefafanuliwa kuwa, baada ya kusikia kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja milango huku wakiomba msaada kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika walifanikiwa kumnusuru mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani.
Majirani kwa hasira walianza kumpiga Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa cheo cha koplo kwa nia ya kumwua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi kazi ya ziada kumnusuru na kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.
Hata hivyo Wakati gari la Poisi likiwa katika mwendo wa kasi eneo la soko la Mkulima, Bwire ameruka kutoka kwenye gari na kuangukia kwenye Lami kitendo kilichomsababishia majeraha makubwa sehemu za usoni.
Mtoto Devotha na baba yake Bwire wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu huku Bwire akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.

MATUKIO KATIKA PICHA
 
MTOTO WA MIAKA 4 DEVOTHA GERLAD ALIYEKATWA MAPANGA NA BABA YAKE,HAPA AKIWA HOSPITALI KWA HUDUMA AYA KWANZA.
  
WANANCHI WAKIWA NJE YA HOSPITALI YA WILAYA WAKIWA NA SHAUKU YA KUMUONA MTUHUMIWA.

KINA MAMA WALIOGUSWA NA TUKIO WAKIWA NJE YA HOSPITALI KUMUONA MTOTO HUYO.

AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI

HAPA AFANDE AKIWA HOI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI..

MADAKTARI WAKIJITAHIDI KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.

MADAKTARI WAKIWA KAZINI KUHAKIKISHA WANAOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.

AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI HUKU AKIWA AMEFUNGWA PINGU.

JITIHADA ZA KUOKOA MAISHA YA MTOTO ZIKIENDELEA

INASIKITISHA SANA JAMANI

MAJUKUMU YA KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO YAKISONGA KWA KASI.

AFANDE BWIRE AKIWA NA PINGU ZAKE WODINI
MUNGU AMPE AHUENI MTOTO HUYU.
source:kijukuublog