Friday, May 17, 2013

GEMU 1500: NI MWISHO KWA LEJENDARI SIR ALEX!


>>JUMAPILI MEI 19: WBA v MAN UNITED, ENZI YA SIR ALEX KWISHA!
>>WANAHABARI WAMTANIA NA KEKI ‘MASHINE KUKAUSHIA NYWELE!’’
FERGUSON_-MIKONO_JUUJUMAPILI, MEI 19, ni Siku ya Mwisho ya Msimu wa BPL, Barclays Premier League, wa 2012/13 na Siku hiyo ndio Mechi ya 1500 kwa Sir Alex Ferguson akiwa Meneja wa Manchester United na ndio mwisho wa enzi yake kwa vile anastaafu.
Akiwa ametwaa Makombe 38 ndani ya Miaka 26 aliyodumu Man United, Sir Alex Ferguson, Miaka 71, amenena: “Ni Mechi 1500…Gemu yangu ya mwisho… inashangaza! Nataka kushinda hii kupita ile ya Wiki iliyopita!”
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
SIR ALEX: MAKOMBE AKIWA MAN UNITED
LIGI KUU: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999, 2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013
FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
UEFA CHAMPIONZ LIGI: 1999, 2008
UEFA KOMBE LA WASHINDI: 1991
FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
UEFA SUPER CUP: 1992
INTER-CONTINENTAL CUP: 1999
FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Jumapili iliyopita Sir Alex Ferguson aliagwa kwa shangwe walipocheza Mechi na Swansea City Uwanjani Old Trafford, ikiwa ni Mechi yake ya mwisho Uwanjani hapo, na kushinda Bao 2-1 na Jumatatu Timu nzima ya Man United ilitembeza Kombe la Ubingwa wa BPL kwenye Mitaa ya Manchester na kusindikizwa na Maelfu ya Washabiki hadi katikati ya Jiji, eneo la Albert Square, walipopokewa na Maelfu ya Umati.
Mwenyewe Ferguson amekiri kuwa mapokezi ya Wiki iliyopita yalishinda yale ya Mwaka 1999 walipopita Mitaani baada ya kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa England, FA CUP na UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, na kuweka Historia ya kuwa Klabu ya kwanza na pekee Uingereza kufanya hilo.
Leo, kwenye Mkutano na Wanahabari kwenye Kambi ya Mazoezi ya Man United huko Carrington ambao ni kawaida ya kila Ijumaa kabla Mechi za Wikiendi, Wanahabari walimpa Sir Alex Ferguson zawadi ya Keki yenye umbo la Mashine ya Kukaushia Nywele ukiwa ni mzaha kuhusu imani ya kwamba Meneja huyo huwapa kibano Wachezaji wake wasipofanya vizuri na kuwafanya wajisikie vichwa vyao moto mithili ya kupitishiwa Mashine hiyo ya Kukaushia Nywele.
Akijibu kwa mzaha, Ferguson alisema: “Inastahili! Kuna wakati sikukubaliana nanyi na kile kilichoandikwa na kuna wakati mliandika vitu vizuri tu na nilividharau. Lakini Siku zote sikuweka kinyongo wala kisasi. Hiyo si staili yangu!”
Ferguson pia alithibitisha kuwa Kipa Anders Lindegaard atakaa Golini Mechi na WBA na Masentahafu watakuwa Jonny Evans na Phil Jones huku Nemanja Vidic na Rio Ferdinand wakiwa Benchi akisisitiza sasa ni zama za Vijana.
+++++++++++++++++++++++
BPL: RATIBA-MECHI ZA MWISHO MSIMU HUU
Jumapili 19 Mei
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Everton
Liverpool v QPR
Man City v Norwich
Newcastle v Arsenal
Southampton v Stoke
Swansea v Fulham
Tottenham v Sunderland
West Brom v Man United
West Ham v Reading
Wigan v Aston Villa
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
**MAN UNITED BINGWA
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Man United
37
43
88
2
Man City
37
33
78
3
Chelsea
37
35
72
4
Arsenal
37
34
70
5
Tottenham
37
19
69
6
Everton
37
16
63
7
Liverpool
37
27
58
8
West Brom
37
-4
48
9
Swansea
37
-1
46
10
West Ham
37
-10
43
11
Stoke
37
-11
41
12
Norwich
37
-18
41
13
Newcastle
37
-22
41
14
Southampton
37
-11
40
15
Fulham
37
-13
40
16
Aston Villa
37
-22
40
17
Sunderland
37
-12
39
18
Wigan *
37
-26
35
19
Reading *
37
-28
28
20
QPR *
37
-29
25
*ZIMESHUKA DARAJA
++++++++++++++++++++++++++++++++++
NI LEJENDARI SIR ALEX FERGUSON
ASANTE SANA NA MOLA AKUBARIKI!!
++NA Storming Fo
Ni mpenzi wa Michezo na maishani mwangu, tangu utoto wangu wako Mashujaa wa Kimichezo, niliowapenda.
Lakini, kimaisha, daima ndani ya moyo wangu ukiondoa Wazazi wangu na Ndugu zangu wa damu, Shujaa mkubwa kwangu na wa pekee ni MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE!!
YEYE, Siku zote husema, HE WAS THE BEST LEADER GOD EVER GAVE A POOR NATION!
Kwenye michezo ni Muhammad Ali.
Wakati Cassius Clay akiibuka ndio enzi hizo hizo England inachukua Ubingwa wa Dunia wakiwa na Wachezaji wa Manchester United Nobby Stiles na Bobby Charlton.
Hiyo ilikuwa Mwaka 1966 na ndio kipindi hicho hicho Cassius Clay akawa Muhammad Ali na Lejendari akazaliwa.
Bobby Charlton, sasa ni SIR BOBBY CHARLTON, mara baada ya yeye na Kaka yake Jackie Charlton aliekuwa akiichezea Leeds United, kuisaidia England kutwaa Kombe la Dunia Mwaka 1966 Uwanjani Wembley, aliandika Kitabu: FORWARD FOR ENGLAND, Kitabu kilichozungumzia maisha yake ikiwemo kunusurika Ajali ya Ndege iliyoua nusu ya Timu ya Manchester United Uwanja wa Ndege wa Munich Mwaka 1958.
Kitabu hicho nilipewa Miaka hiyo hiyo kilipotoka na Kaka yangu, Baba mmoja Mama mmoja ‘aliesaliti’ Ukoo wetu kwa kuichezea Sunderland, sasa ndio hii Simba, wakati Ukoo wetu ni Yanga damu.
Mie baadae nilihamia Pan Africans lakini hadi hii leo Simba, si Yanga, ni ‘adui’ kwangu!
Kitabu hicho, FORWARD FOR ENGLAND, kilinifanya niipende Manchester United tangu wakati huo hadi hii leo.
Niliifuatilia sana Man United kupitia Magazeti na BBC, ikishuka Daraja na kupanda tena, hadi Novemba 1986 alipotua Mtoto wa Kuli wa Poti ya Govan, Alex Ferguson, kuleta Mapinduzi.
Kuanzia hapo hadi sasa, wanavyosema Wahenga ni Historia!
Manchester United iliibuka na kusambaratisha Timu zote England, hasa Liverpool waliokuwa Wababe, kutetemesha Ulaya na Dunia na kukubalika kuanzia huko Manchester, kila kona ya Dunia hadi kule kwetu Samvula Chole.
Yote ni kazi ya Alex Ferguson, sasa ni SIR Alex Ferguson!
Upo wakati nilikufurahia sana, upo wakati ulinichukiza, hasa staili yako ya kubadilisha Wachezaji kila Mechi kupindukia, kitu ambacho wakati mwingine kilileta madhara, lakini kila wakati ulidhihirisha wewe ni MSHINDI!
UNASTAHILI HESHIMA, SIR ALEX FERGUSON!
NAKUTAKIA KILA LA HERI MAISHA YAKO YA BAADAE!
ASANTE SANA NA MOLA AKUBARIKI!!
BILA KUPINGWA,
WEWE NI LEJENDARI!!

No comments:

Post a Comment