Mapenzi ni kitu Fulani tofauti sana kwenye hii dunia na hata nje ya
hii sayari. Mapenzi kwa kiasi kikubwa sana yanasababisha hata mambo mengine
kwenye hii dunia yaende sawa au yaende tofauti hata kama hayahusiani na
mahusiano ya mapenzi. Vifo vingi hutokana na mapenzi, kuna magonjwa watu
wanaumwa kisa mapenzi, kuna mambo watu wanayafanya si ya kawaida kisa mapenzi.
Ukiachilia mbali PESA, Mapenzi huwa yana nafasi kubwa sana kwenye
kitu chochote ndani yahii dunia tunayoishi. Si masikini wala si tajiri, wote
kwa pamoja wanahitaji mapenzi kutoka kwa wanaowapenda ili dunia iweze kwenda
sawa kwa upande wao. Na ndio sababu hata mimi hapa ninaandika kuhusu mapenzi
kwa sababu yananigusa hata mimi na hata wewe unayesoma hapa sasa.
Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe ya
tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele kwako
kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa
sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.
Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au kutojaliwa kama wewe unavyojali
basi hata dunia iwe na raha gani kwako utaiona chungu na hata raha ya maisha
hutakuwa nayo hata kama una hela kiasi gani na hata kama una cheo kikubwa kama
mfalme au hata rais. Wengine hufikia hatu ya kuteseka tu bila kuondoka kwenye
mahusiano kwa kuogopa kuumizwa tena huko waendapo na wengine huondoka baadae
sana wakiwa tayari wameshachelewa.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua
kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Mojawapo
kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;-
1. UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote
ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na
uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana hasa kama mmojawapo
akigundua kuwa mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
Kuna vitu vingine hata kudanganyana haileti maana wala haina tija
kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni jambo jema sana kuliko
kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua unamdanganya itakuwa matatizo na
unaweza kusababisha kuachana.
2. USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni pamoja na hili la
usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye mapenzi/mahusiano bora
kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa
moja. Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya
moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta
ugomvi au matatizo hao baadae.
Kama kuna kitu hukuwahi kumwambia na unahisi ukimwambia atakasirika
ni bora umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko aje kugundua mwenyewe itakuwa
shida sana kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye mahusiano mwaka wa 4 sasa na kumbe
kabla ya kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una watoto 2 kwa huyo mke/mume
wa mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza kukuelewa lakini mara
nyingi ni kwa shingo upande.
3. ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye love kama kugundua kuwa Yule unayempenda
tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana mtu mwingine
zaidi ya wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha hata wengine kuweza
kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa bado wanapenda pale walipo. Hakuna
binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye mapenzi.
Kamwe Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye Ajutie Penzi
Lako, Usimfanye Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni Ujanja Lakini
Ipo Siku Utahitaji Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata, Laana Ya
Mapenzi Ipo, Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi Ya Kweli Yaanawezekana
Kma Ukiamua na si kwa ku-cheat.
4. DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama sio
kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa
khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake
au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.
Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya
wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri au hata
akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya
wapenzi wao kiuwezo, ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa Linapokuja Suala La
Ndoa/Kuishi Na Mtu, Kwetu Sie Wanaume Huwa Hatuangalii Uzuri/Urembo Wa Mwanamke
Kama Ndio Kigezo Pekee Cha Kufanya Tumuoe/Tuishi Na Huyo Mwanamke, Ingekuwa
Hivyo Basi Wanawake Wote Warembo/Wazuri Wangekuwa Ndani Ya Ndoa Leo Hii, Hii
Inamaanisha Kuwa Hata Ukiwa Mrembo/Mzuri Hutakiwi Kujisahau Ukaona
Umeshafika...Utapotea ukileta dharau kwa uzuri wako au uwezo ulionao.
5. MROPOKAJI/ASIYE MSIRI.
Hakuna kitu kinachoweza kumfanya mwenza wako kukukimbia au hata kukosa
uaminifu na wewe kama akija kugundua kama wewe ni mropokaji na huna ‘’kifua’’
hasa kwa yale mambo ambayo ni ya chumbani na hayakutakiwa kutoka nje. Hakuna
mtu anayependa siri zake kutoka hadharani na huwa inaumiza sana kwenye mapenzi
kumpa mtu siri zako then yeye anaenda kusimulia.
Mambo mnayafanya mkiwa wawili tena ndani lakini kesho unaenda
mtaani unakuta kila mtu anajua mlichofanya tena wanakuhadithia kama walikuwepo
vile, hiyo si kitu nzuri na itakufanya ukimbiwe na kila mpenzi unayempata.
6. TAMAA/KUKOSA UVUMILIVU.
Tamaa ni kitu kingine ambacho hufanya mahusiano mengi kukosa nguvu
na mengine kuvurugika kabisa. Kama mpo kwenye mapenzi na mmeamua kupendana kwa
shida na raha basi haitakiwi mmoja wenu kuwa na tama na kukosa uvumilivu hata
kwa yale mambo yanayoweza kuzuilika.
Kama mpenzi wako ni wa hali Fulani na umeamua kuwa naye basi usiwe
na tama kwa vitu vingine ambavyo vinaweza kukusababishia mahusiano yako kukosa
nguvu na kufa kabisa. Amini kuwa ipo siku mtakuwa na vitu kama unavyotamani kwa
kuongeza bidii kutafuta na kushauriana nini cha kufanya lakini si kwa kutafuta
‘’shotcut’’/njia nyepesi nyepesi zinazoweza kuku-cost hapo baadae.
7. KUKOSA MSIMAMO.
Hii kitu huwakuta wengi sana kwenye mapenzi ya siku hizi. Nadhani
ni hali halisi ya dunia ya sasa inachangia pia pamoja na teknolojia tuliyonayo
ya kutuwezesha kufanya yale tunayoyaona kwenye mitandao na vyombo mbali mbali
vya habari.
Wapenzi wengi siku hizi wamekosa msimamo kwenye mapenzi/mahusiano
yao na unakuta tu mmoja anakuwa na wapenzi zaidi ya mmoja na wanakuwa
hawafahamiani huku kila mmoja akijua kuwa yeye ndo kila kitu kwa mpenzi wake.
8. KUTOJALI/KUTOKUWA NA
MSAADA.
Hii pia kwa kiasi kikubwa inaumiza sana na kupelekea kushuka kwa
thamani ya mapenzi miongoni mwa mahusiano mengi haa duniani. Kama kweli
unampenda mpenzi wako basi msaidie anapopata matatizo na umjali na kumchukulia
kama mpenzi wako na mtu wako wa karibu na sio kukimbia majukumu bila sababu
zote za msingi.
Kama huwezi kujali na kusaidia basi usiingie kwenye mahusiano ni
bora ukae mwenyewe kuliko kuwepo sehemu usiyotakiwa.
9. UBAHILI.
Huna sababu yoyote ya kuwa na pesa na mpenzi wako akawa anapata
tabu kama vile humuoni. Sijasema utoe pesa hata kwa mambo yasiyo na msingi
lakini at least utimize majukumu yako kwa mpenzi wako kila unapohitajika.
Kuna vitu vingine hata huhitaji kuambiwa kama unatakiwa
kuvishughulikia, ni wewe mwenyewe tu kuwa responsible kumhudumia mpenzi wako.
Na hii huwa ina-apply sana kwa wavulana kutokana na kasumba iliyojengeka na
mila tulizozikuta.
10. USHOGA/USAGAJI
Hii ipo wazi kabisaaaaaaa…. Hakuna mtu anayependa mtu wake awe
Shoga kama ni mvulana au awe Msagaji kama ni msichana. Ni aibu kubwa sana kwa
mpenzi wako kuwa katika makundi haya mawili na sidhani kwa akili ya kawaida
kama unaweza kufurahia hiki kitu kama utakisikia au kama utakishuhudia kwa
macho yako.