Kamati kuu na halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi {NEC}
zimekutana mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine vikao hivyo
vimejadili mchakato wa bunge la katiba na kubainisha mafanikiano ya
upatikanaji wa katiba mpya kati ya Rais Jakaya Kikwete na vyama vya
siasa vinavyiunda kituo cha Demokrasia Tanzania {TCD} hayazuii chama
hicho kuendelea na mchakato wa katiba.
Vikao hivyo vikuu vya CCM katika ngazi za mbali na kujadili
mchakato wa bunge maalum la katiba pia vimezungumzia mustakabali wa
chama hicho katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu
huku katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho Nape Nauye akisema
wataendelea kujadili katiba kwani ajenda za TCD sio ajenda za CCM kwa
kuwa vikao vyake vinajitegemea na viko huru.
Akizungumzia msimao wa chama hicho kuhusu kura za maoni ya wananchi
Nape amesema CCM itaendelea kuheshimu sheria ya mabadiliko ya katiba ya
mwaka 2012 sura ya 83 inayoelekeza kura za maoni zipigwe ndani ya siku
84 baada ya bunge maalum kuvunjwa lakini pia akisisitiza sheria hiyo
inaweza kufanyiwa mabadiliko na bunge la jamuhuri ya muungano wa
Tanzania.
No comments:
Post a Comment