Saturday, November 22, 2014

Home MSANII KAJALA AFUNGUKA JUU YA YEYE KUZAA TENA

MWIGIZAJI Kajala Masanja amefunguka kuwa anatamani kuongeza mtoto wa pili kwani tayari aliyenaye ameshakua vya kutosha. 

Mwigizaji wa filamu Bongo, Kajala Masanja akiwa na mwanaye Paula.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Kajala alisema anasaka mimba kwa namna yoyote ili mwanaye Paula apate mdogo wake hivyo suala hilo lipo katika mchakato yakinifu na mpenzi wake wa sasa ambaye hakupenda kumwanika jina lake.
Kajala Masanja akipozi.
Natamani kuongeza mtoto wa pili, Paula ameshakua mkubwa lazima tumtafutie mdogo wake mambo ndiyo yatakuwa mazuri zaidi,” alisema Kajala.Mtoto huyo wa awali, Kajala alizaa na prodyuza Paul Matthysse ‘P Funk’ ambaye walishamwagana.

No comments:

Post a Comment