Kijana
ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiugulia maumivu baada ya
kupokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kwa kile
walichomtuhumu kuiba simu katika moja ya duka lililopo maeneo ya
Makumbusho karibu na Kituo cha Daladala, jijini Dar es Salaam.
Wakielezea
tukio hilo mashuhuda walisema kuwa kijana huyo aliingia katika duka
hilo lililokuwa na mwanadada na kupora simu iliyokuwa juu ya kabati la
bidhaa na kutimka nayo jambo lililomfanya mwanadada huyo kutoka nje na
kuanza kupiga kelele za kuomba msaada.
Kama
ilivyo kawaida kijana huyo aliangushiwa na kila mtu aliyemuona akitimka
na kufanikiwa kumtia nguvuni na kuanza kula kichapo hadi aliporejesha
simu ya mdada huyo. Baadaye aliachiwa huru na kuondoka zake.




No comments:
Post a Comment