Stori: Gladness Mallya
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa japokuwa ana watoto wengine wa
nje lakini anajivunia kuzaa na mkewe, Siwema kwani walipitia changamoto
nyingi kabla ya kupata mtoto.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Nay
alisema katika maisha ya mapenzi yake na Siwema walivumilia vingi na
hivi sasa ana mshukuru Mungu kwani wameweza kufikia hatua nzuri ya
kupata mtoto.
“Maisha ya mapenzi yetu yalikuwa na changamoto
sana lakini nilisimama kwa sababu nampenda mke wangu Siwema, najivunia
kuzaa na Siwema mtoto wa kiume na ninaendelea kumuomba Mungu aendelee
kumkuza mwanetu,” alisema Nay wa Mitego.
Wadau mbalimbali wamekuwa wakimpongeza Nay kwenye mitandao ya kijamii
kwa kile wanachodai kwamba ana mapenzi ya kweli licha ya changamoto
nyingi zilizojitokeza kwa mpenzi wake Siwema za picha kuzagaa mitandaoni
kwamba alikuwa mchumba wa mtu.
No comments:
Post a Comment