BAADA ya hivi karibuni Msanii wa Filamu na Muziki Bongo, Baby Madaha
kusema ameamua kuwapanga wanaume, hivi sasa ameibuka na jipya na kudai
kwamba huwa hatumii kinga ‘kondom’ hata siku moja.
Akipiga stori na paparazi wetu, Baby Madaha alisema kabla hajaanguka
penzini na mwanaume lazima akapime kwanza Ukimwi na baada ya hapo ndipo
mambo mengine yanaendelea hivyo akishahakikisha huyo mwanaume ni mzima
huwa ahangaiki kutumia kinga.
“Japokuwa nawapanga wanaume lakini najali sana afya yangu yaani kila
baada ya miezi mitatu huwa naenda kupima kabla sijaingia naye kwenye
uhusiano, nikikuta yuko fresh tunaendelea na mapenzi yetu na huwa
situmii kinga kwa sababu nakuwa nimeshajua afya yake.
Ikitokea amenizingua nampiga chini namchukua mwingine naenda kumpima hivyohivyo maisha yanasonga mbele,” alisema Baby Madaha.

No comments:
Post a Comment