Dear Admin,
Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuendesha page hii, na umahiri wenu ndio umenisukuma leo hii nijitokeze hapa nikiomba
ushauri kwa wasomaji wenu mahiri na wenye kustaarabika, maana huwa hakuandikwi mambo ya ajabu ajabu hapo.
Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 24, nina mpenzi wangu ambaye hivi sasa tuna miezi takriban minne toka tuanze mahusiano yetu.
Ni kijana mtanashati na mwenye kujimudu kwa upande wa kipato na kwakweli amekuwa msaada mkubwa sana kwangu na kwa familia
yangu pale ambapo nimekuwa nikimshirikisha, ingawa sio sana kwasababu
nami namiliki biashara zangu na zinanitosheleza kimahitaji ya lazima kwa
ujumla.
Tatizo langu sasa kwa huyu mpenzi ni kuwa, yeye anapenda sana kushiriki
tendo la ndoa. Yaani karibu kila siku yeye anataka tufanye
hicho kitu na ikitokea siku hiyo anataka na niko kwenye mzunguko wa zile
siku za wanawake, basi hunilazimisha tufanye hata kwa kutumia mpira.
Tabia hii kwakweli imekuwa ikinikera sana, maana ni kama vile anataka
kunitumia tu kama chombo chake cha starehe na wala sio kama mwenza wake
na ninayehitaji pia kujaliwa. Kilichonisukuma kuibuka kuomba ushauri leo
hii ni kwamba, wiki jana nilikuwa kwenye siku zangu, na kama ilivyokuwa
ada ya jamaa, akanijia siku hiyo akitaka tufanye mapenzi, mie
nikamkatalia katakata maana nishaona
namuendekeza sana, unajua alinijibu nini, eti “kama unaona unaumia
kufanya hivyo ukiwa kwenye siku zako, basi uwe unanipa penzi kinyume cha
maumbile” kha!!
Yaani niliishiwa nguvu, nikajiondokea zangu kwake na kwenda kwa rafiki
yangu ambako niko hadi leo. Sasa najiuliza, huyu mwenzangu ana akili
timamu kweli?
Je, ananipenda au anataka kunitumia tu? Au ana ugonjwa fulani labda
wataalamu wa tiba waniambie. Natanguliza shukrani, naamini nitashauriwa
juu ya hili.

No comments:
Post a Comment