Namna ya kumsahau mpenzi wako wa kwanza
Kuachana na wapenzi wa kwanza huumiza, wakati mwingine vigumu
kupona vidonda vyake wengi huyumba sana kimahusiano wanapopata wapenzi
wapya. Hizi ni baadhi ya hatua za kuchukua ili umsahau mpenzi wako wa
kwanza, usonga mbele;
1. Kata mawasiliano, hakikisha hakuna mawasiliano ya aina yoyote iwe ni simu, fb, au outings na ex wako
2. Kumbuka ulichokichukia sana kwa ex wako, yote mabaya au mapungufu
yake yatakufanya uone umetua mzigo mzito katika maisha yako.
3. Amini kuwa kila kitu hutokea kwa mpango wa Mungu na kuwa atakuwa amekupangia kizuri zaidi ya ulichokipoteza
4. Uwe wazi, zungumza na marafiki na ndugu kupunguza msongo
5. Punguza au acha kabisa kutumia zawadi zake; nguo, saa au vitu vinavyoweza amsha kumbukumbu yake.
Omba sana Mungu ukijua kila kitu kitapita isipokuwa yeye aliye juu ya vyote, atakupa aliyekupangia.
No comments:
Post a Comment