Binti akijiachia na njemba huyo baada ya kupiga urabu wa kutosha.
Stori: Richard Bukos ULEVI
noma! Ndivyo unavyoweza kusema kuhusu kilichomtokea mtoto wa kigogo
mmoja aishie Masaki ambaye alijikuta akifanyiwa kitu mbaya ndani ya maji
kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Coco jijini Dar, Jumamosi
iliyopita.
Kabla ya tukio hilo, inadaiwa kuwa dada huyo ambaye jina lake
halikuweza kufahamika mara moja, alikesha katika klabu moja iliyopo
ufukweni hapo, akipiga ulabu yeye pamoja na kampani yake.Ilipofika
asubuhi, inadaiwa kuwa, ili kupunguza ulevi aliokuwa nao kichwani,
aliamua kwenda kuogelea, ili akae sawa.
Chanzo kilichoshuhudia tukio hilo kilishadadia maneno kwa mpigapicha
wetu kwa kusema kuwa, wakati mrembo huyo anaenda kuogelea ndipo
alipoangukia kwenye mikono ya njemba mmoja aliyekuwa akifanya mazoezi
pembeni mwa ufukwe huo ambapo pia alikutana na wachezaji wa Azam FC
waliokuwa wakifanya mazoezi mambo yakaharibika.
“Wakati anawafuata wale wachezaji, redio za watu wa bajaj zilikuwa
zimefungulia muziki kwa sauti, akawa anacheza, jamaa walipoona vile
wakaongeza sauti na kumwekea wimbo wa Davido wa Aye, dah, ndio
akachizika kabisa, jinsi alivyokuwa akikata mauno na nguo alizovaa,
aliwachanganya kabisa wachezaji wa Azam ambao walikuwa wakimtumbulia
macho kwa udenda,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuwapagawisha wachezaji hao, binti huyo alipomfuata njemba
mmoja aliyekuwa kando na kumuomba amfundishe kuogelea, jamaa akachukua
tairi la gari na kumwingiza baharini ambako alianza makeke ya
kumfundisha huku wakizamia kuonesha kuna kamchezo kachafu kanaendelea.
Baadaye
akiwa kama aliyeshtuka, alikurupuka majini humo na kutoka nje
akikimbia, akimuacha njemba aliyekuwa naye baharini akimtumbulia macho
ya kutoamini kilichotokea.
No comments:
Post a Comment