Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema anayedaiwa kutoroshwa na mchungaji huyo.
Mchungaji
anayejiita nabii na mtume, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
(DRC) aliyetajwa kwa jina moja la Emmanuel amejikuta ndani ya majanga
kufuatia madai mazito kwamba amemtorosha mke wa mtu ambaye ni mwimbaji
wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, mchungaji huyo alifika nyumbani kwa Jonas
Mrema, mume wa Janet, maeneo ya Tegeta-Nyaishozi jijini Dar na kuishi
kama mtumishi wa Mungu lakini polepole alianza mazoea tata na Janet.
“Mume
alianza kuhisi mabadiliko ya mkewe kwa mtumishi huyo, lakini nadhani
aliona ni mawazo yake tu. Ndipo siku ya siku akashangaa mkewe na
mchungaji huyo wameondoka nyumbani hapo.
“Kwa sasa tangu tukio hilo litokee ni miezi kama mitatu. Mume alihangaika sana kumtafuta mkewe hadi jana (Jumatatu iliyopita) ndipo akampata wakiwa na mchungaji huyo kwenye nyumba moja ambako walikuwa wakiishi pamoja,” kilisema chanzo chetu.
Iliidaiwa
kwamba, mchungaji huyo alipopekuliwa alikutwa na paspoti ya nchini
Burundi wakati yeye ni Mkongo wa Uvira na alionekana kuishi nchini
kinyume na sheria hivyo alifunguliwa jalada la kesi kwenye Kituo cha
Polisi cha Wazo Hili, Tegeta lenye Kumbukumbu Na. WH/RB/7040/2014- KUISHI NCHINI BILA KIBALI.
Juzi, Amani liliwasiliana na Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela Joel ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari chama hicho kimemsimamisha uanachana Janet kwa kitendo chake hicho cha kumtoroka mumewe wa ndoa.
“Ni kweli na Chama cha Waimba Injili Tanzania kimemsimamisha uanachama Janet. Hatuna mzaha katika maadili,” alisema Stela.
Amani
lilimpigia simu mume wa Janet, Jonas Mrema ambapo katika mazungumzo
baada ya salamu alipewa pole kwa matatizo ya mkewe, alisema asante kisha
alipoulizwa kuhusu hali ilivyo aliomba apige simu yeye baadaye kwa vile
alikuwa kikaoni.
Hata
hivyo, baada ya saa mbili kupita bila kupiga, Amani lilimpigia tena
simu ambapo iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata
zinaendelea.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment