Wanawake wawili kutoka familia moja wakazi wa kitongoji cha Nanzilo kijiji cha Ihugi,kata ya Lyamidati tarafa ya Nindo wilaya ya Shinyanga vijijini wameuawa kikatili baada ya kuchinjwa kwa panga na watu wasiofahamika wakati wakijiandaa kula chakula cha usiku.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha amesema tukio hilo
limetokea Oktoba 14 mwaka huu saa mbili usiku na kuwataja wanawake waliouawa kuwa ni Dilu Tungu(80) na mtoto wake Bunya Mihangwa(45).
Kamanda
Kamugisha amesema wanawake hao wakiwa wakijiandaa kula chakula cha
usiku na wanafamilia wenzao ghafla walivamiwa na watu watatu
wasiofahamika kisha kuanza kuwakata kwa panga sehemu
mbalimbali za miili yao kisha kuwachinja shingo hadi wakapoteza
maisha.
Chanzo cha tukio hilo kinatajwa kuwa ni
imani za kishirikina kwani kuna mwanamme aitwaye Bwanya
Mlyashimba(40) (ambaye anashikiliwa na polisi) mkazi wa Ihugi alikuwa akiwatuhumu marehemu hao kwamba walimroga
yeye na kusababisha akose nguvu za kiume na kwamba walimroga
mama yake Hollo Mahangwa aliyefariki dunia mwaka
2013.
Tayari Bwanya Mlyashimba anashikiliwa na jeshi la polisi watuhumiwa wengine wanasakwa.
Tayari Bwanya Mlyashimba anashikiliwa na jeshi la polisi watuhumiwa wengine wanasakwa.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment