Friday, October 17, 2014

USHIRIKINA WASABABISHA WANAWAKE WAWILI WA FAMILIA MOJA KUCHINJWA HUKO SHINYANGA



Wanawake wawili kutoka familia moja wakazi wa kitongoji cha Nanzilo kijiji cha Ihugi,kata ya Lyamidati tarafa ya Nindo wilaya ya Shinyanga vijijini wameuawa kikatili baada ya kuchinjwa kwa panga na watu wasiofahamika wakati wakijiandaa kula chakula cha usiku.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea Oktoba 14 mwaka huu saa mbili usiku na kuwataja wanawake waliouawa kuwa ni Dilu Tungu(80) na mtoto wake Bunya Mihangwa(45).

Kamanda Kamugisha amesema wanawake hao wakiwa wakijiandaa kula chakula cha usiku na wanafamilia wenzao  ghafla walivamiwa na watu watatu wasiofahamika kisha kuanza kuwakata kwa panga sehemu mbalimbali za miili yao kisha kuwachinja shingo hadi wakapoteza maisha.

Chanzo cha tukio hilo kinatajwa kuwa ni imani za kishirikina kwani kuna mwanamme aitwaye Bwanya Mlyashimba(40) (ambaye anashikiliwa na polisi) mkazi wa Ihugi alikuwa akiwatuhumu marehemu hao kwamba walimroga yeye na kusababisha akose nguvu za kiume na kwamba walimroga 
 mama yake Hollo Mahangwa aliyefariki dunia mwaka 2013.
Tayari Bwanya Mlyashimba anashikiliwa na jeshi la polisi watuhumiwa wengine wanasakwa.

No comments:

Post a Comment