Wimbi la matukio ya kinyama dhidi ya walemavu wa ngozi yameendelea
kushamiri katika maeneo mbalimbali hapa nchini hususani Mikoa ya Kanda
ya Ziwa na kila kukicha bado taarifa zimeendelea kutolewa huku bado
ufumbuzi ukionekana kutofikiwa muafaka.
Pamoja na adhabu ambazo hutolewa na vyombo vya dola dhidi ya wahusika
lakini imeonekana kama sikio la kufa kwani bado tunaendelea kushuhudia
matukio yanayofanana na hayo yakishamiri ndani ya jamii
Mmoja wa waliokua wakifanya biashara haramu ya ngozi za binadamu
aliyenusurika adhabu ya kunyongwa mwaka 2002 ambaye hakutaka kutaja jina
lake amekutana na Gazeti la MTANZANIA na kufichua siri za namna biashara hiyo inavyofanyika hapa nchini kwa usiri mkubwa huku kukiwa na mtandao mkubwa ndani yake.
Sambamba na hilo pia ameelezea jinsi wanamtandao wa biashara ya ngozi
walivyosambaa katika nchi jirani ambao hushiriikiana katika biashara
hiyo.
Akitokea Mkoa wa Mbeya alisema alianza biashara hiyo toka mwaka 1997
baada ya kuacha biashara ya baa ambapo alikutana na wafanyabiashara wa
ngozi za binadamu toka sehemu mbalimbali.
Alisema wateja wao wakubwa walikua ni matajiri wanaomiliki migodi
ambao maskani yao ni porini pamoja na majamba ambao hata hivyo hajui
walikua wakizipeleka wapi na kufanyia shughuli gani kwa wakati huo.
Alisema biashara hiyo ni ngumu sana kwani unatakiwa kuwa jasiri sana
na hufanyika kwa usiri mkubwa ambapo huua watu na kisaha kuwachuna ngozi
kabla ya kwenda kuziuza kwa bei nzuri ambayo hakua tayari kuiweka
hadharani.
Alisema aliponea kunyongwa na mpaka sasa hajui aliachiwaje huru huku
akikaa gerezani kwa miaka minne na alikutana na mateso ya aina yake huku
akizimia kwa siku mbili mfufulizo bila msaada wowote kutokana na kipigo
na wenzake wanne wakaishia adhabu ya kunyongwa.
No comments:
Post a Comment