Tuesday, December 23, 2014

UNAPOMKUTA MPENZI WAKO KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA INAKUPASA UFANYE HIVI!


Habari za mida wanakisiwa! Sikuzote katika mapenzi wivu ni chachu ya upendo, Mapenzi bila wivu ni sawa na chai bila sukari, Kama kweli unampenda mpenzi wako kwa moyo mmoja tena kwa dhati haipiti siku hamjaonana wala haipiti saa haujaenda hewani wala kumtumia sms lazima uwe na wivu kwake.

Hapo hapo wivu ni ni sumu katika mapenzi nasema ni sumu kwa sababu wivu ukizidi huwa kero kwani kila wakati utakachokiona kwa mpenzi wako lazima uje juu , Hapo inatakiwa uwe mpole umsubiri akirudi nyumbani pia umwaangalie yupo katika hali gani, wakati huo umwandalie kile chakula akipendacho au umtoe Out namwende  sehem iliyotulia Sio bar tena.

Baada ya kufika agiza kile akipendacho na mwagizie na yeye au muulize ungependa ni kuagizie nini mpenzi. Wakisha leta usimwachie muudumu ndie amkaribishe wewe mwambie tuwekee hapo tunashukuru wewe endele nakazi zako
Hapo sasa kazi inaanza .......... nafasi ni yako mkaribishe wewe mwenyewe mwambi mpenzi karibu lazima ajisikie faraja sana na lazima ajihisi yeye ni wapekee kwako hakuna mwingine zaidi yake. Ikiwezekana kama ni chakula chukua kijiko mlishe na kama nikinywaji mwenyweshe kwa madaa...... wacha weweeee..................

Kazi inaanza huwezi kujenga nyumba bila kuanza kujenga msingi kwanza au vipi. Nadhani utakuwa umenelewa na maanisha nini hadi hapo au vipi wanakisiwa. Anzia kupiga story nzuri zile za wakati huo au mazuri aliyo kwisha tenda kwako kisha mwambie mabaya aliyokwisha tenda kwako kwa upole na taratiiiiiibu.

Lazima uone kitu flani katika macho yake au usoni mwake iwe isiwe lazima utaona mabadiriko katika sura yake , hata awe kauzu vipi zaidi ya dagaa lazima akuombe msamaha kwa yale aliyotenda kwako, Endelea na kusifia ama kupongeza tena kwa mazuri mengine aliyokwisha fanya kwako kwa mala nyingine.
Baada ya hapo hatua inayofuaata kwa utaratibu na huku ukichombweza maneno matamu, kwa mfano umemuona na msichana au mwanaume au Mazingira uliyomuona sio mauzuri inakubidi uanze sasa.

Hapa unaanza ’’ mpenzi mimi huwa na wivu hasa pale napokuona upo na mwanaume/mwanamke au napokukuta mazingira ya kutatanisha  hii yote sababu nakupenda spendi ufanye hivyo kwani unaumiza moyo wangu mpenzi ’’. Hapo msikilize atakujibu vipi au atasema yapi juu ya kile ulichomwambia , baada ya majibu yake ndipo umwambie alafu leo nimekuona ulikuwa na msichana/mwanaume ama mazingira uliyokuwepo leo sijayapenda.

Hapo hata kama alikuwa mkorofi vipi lazima akuambie na kama ni mkweli lazima aseme ukweli awezi kukuficha kitu kutokana na jinsi ulivomuuliza, Ukiona amekweleza majibu utata usikazanie kuhoji mwache, mvizie hadi pale mnapokuwa katika ulimwengu wa raha .Hapo mweleze kuwa lile jibu ulilonipa sikulizika nalo mpenzi kwani na mashaka.

No comments:

Post a Comment