Habari za
mida wanakisiwa! Sikuzote katika mapenzi wivu ni chachu ya upendo, Mapenzi bila
wivu ni sawa na chai bila sukari, Kama kweli unampenda mpenzi wako kwa moyo
mmoja tena kwa dhati haipiti siku hamjaonana wala haipiti saa haujaenda hewani
wala kumtumia sms lazima uwe na wivu kwake.
Hapo hapo wivu
ni ni sumu katika mapenzi nasema ni sumu kwa sababu wivu ukizidi huwa kero
kwani kila wakati utakachokiona kwa mpenzi wako lazima uje juu , Hapo inatakiwa
uwe mpole umsubiri akirudi nyumbani pia umwaangalie yupo katika hali gani,
wakati huo umwandalie kile chakula akipendacho au umtoe Out namwende sehem iliyotulia Sio bar tena.
Baada ya
kufika agiza kile akipendacho na mwagizie na yeye au muulize ungependa ni
kuagizie nini mpenzi. Wakisha leta usimwachie muudumu ndie amkaribishe wewe
mwambie tuwekee hapo tunashukuru wewe endele nakazi zako
Hapo sasa
kazi inaanza .......... nafasi ni yako mkaribishe wewe mwenyewe mwambi mpenzi karibu
lazima ajisikie faraja sana na lazima ajihisi yeye ni wapekee kwako hakuna
mwingine zaidi yake. Ikiwezekana kama ni chakula chukua kijiko mlishe na kama
nikinywaji mwenyweshe kwa madaa...... wacha weweeee..................
Kazi inaanza
huwezi kujenga nyumba bila kuanza kujenga msingi kwanza au vipi. Nadhani
utakuwa umenelewa na maanisha nini hadi hapo au vipi wanakisiwa. Anzia kupiga
story nzuri zile za wakati huo au mazuri aliyo kwisha tenda kwako kisha mwambie
mabaya aliyokwisha tenda kwako kwa upole na taratiiiiiibu.
Lazima uone
kitu flani katika macho yake au usoni mwake iwe isiwe lazima utaona mabadiriko
katika sura yake , hata awe kauzu vipi zaidi ya dagaa lazima akuombe msamaha
kwa yale aliyotenda kwako, Endelea na kusifia ama kupongeza tena kwa mazuri
mengine aliyokwisha fanya kwako kwa mala nyingine.
Baada ya
hapo hatua inayofuaata kwa utaratibu na huku ukichombweza maneno matamu, kwa
mfano umemuona na msichana au mwanaume au Mazingira uliyomuona sio mauzuri
inakubidi uanze sasa.
Hapa unaanza
’’ mpenzi mimi huwa na wivu hasa pale napokuona upo na mwanaume/mwanamke au
napokukuta mazingira ya kutatanisha hii
yote sababu nakupenda spendi ufanye hivyo kwani unaumiza moyo wangu mpenzi ’’.
Hapo msikilize atakujibu vipi au atasema yapi juu ya kile ulichomwambia , baada
ya majibu yake ndipo umwambie alafu leo nimekuona ulikuwa na msichana/mwanaume
ama mazingira uliyokuwepo leo sijayapenda.
Hapo hata
kama alikuwa mkorofi vipi lazima akuambie na kama ni mkweli lazima aseme ukweli
awezi kukuficha kitu kutokana na jinsi ulivomuuliza, Ukiona amekweleza majibu
utata usikazanie kuhoji mwache, mvizie hadi pale mnapokuwa katika ulimwengu wa
raha .Hapo mweleze kuwa lile jibu ulilonipa sikulizika nalo mpenzi kwani na
mashaka.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment