Muuza nyago kwenye sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’.
Mamaaa! Muuza nyago kwenye sinema za
Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ ameibuka na kuanika kijasiri kuwa
‘ameshambonji’ na mastaa wa kiume 15 wa Bongo huku akisema kitendo hicho
hakijamuondolea hadhi yake, Risasi Mchanganyiko linatiririsha.
Akizungumza katika mahojiano maalum na
waandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar, Bozi alitamka
hayo kwa kujiamini zaidi.Mahojiano kati ya msanii huyo na Risasi
Mchanganyiko yalikuwa kama ifuatavyo:
Risasi: “Mzima Bozi?”
Bozi: “Mi mzima sana. Enhe! Karibuni maana nasikia mmenitafuta sana, kuna nini?”
Risasi: “Tumeshakaribia. Sisi tunataka kufanya mahojiano na wewe kuhusu sanaa kwa ujumla, ugumu na wepesi wake.”
Bozi: “Oke, sawa.”
Risasi: “Oke,
labda kwa kuanzia Bozi, umeshapambana na ugumu wowote kwenye fani? Kama
vile kulazimishwa kuvaa nguo za hasara kutokana na ‘sini’ unayoigiza?”
Bozi: “Bahati nzuri nguo tunazovaa kwenye ‘viwanja’ kujirusha ndizo hizohizo hata tunazovaa mtaani. Kwa hiyo hakuna ugumu wowote.”
Risasi: “Wasanii mnaoibukia siku hizi mnadaiwa mmevamia fani ili kuuza sura na kutafuta mabwana, hasa mapedeshee. Kuna ukweli?”
Bozi: “Pengine
wapo lakini mimi nimeingia kwenye fani kwa sababu ya msukumo wa kipaji
changu na si kutafuta mabwana. Kama mabwana mbona wapo mastaa kibao
nilishalala nao kabla.”
Risasi: “Ziko
habari kwamba, kila msanii mdogo Bongo anapoingia kwenye fani, ili
atoke sawa lazima awe amegawa penzi kwa mastaa wakubwa, madairekta au
maproduyza. Vipi wewe, imekutokea hiyo?”
Bozi: “Hapana! Sijawahi kuombwa penzi.
Ila kama nilivyosema, mapenzi yapo ndiyo
maana nikasema kuna mastaa wakubwa tena wenye levo ya juu Bongo
nimeshalala nao lakini si kwa sababu ili nitoke, walinipenda tu.”
Risasi: “Hebu tubaki hapo kwa muda! Hao mastaa unaweza kuwataja kwa majina?”
Bozi: “Sidhani kama nitaweza, lakini ni mastaa wakubwa, si wa filamu tu, wengine ni wa Bongo Fleva. Tena wapo ambao ni waume za watu.”
Risasi: “Wangapi?”
Bozi: “Hao
waume za watu au mastaa kwa ujumla. Kama ni mastaa wote niliowahi
kulala nao ni kumi na tano.“Lakini naomba ijulikane na jamii kwamba,
hiyo haiwezi kushusha hadhi yangu. Kibaya ni kama ningekuwa nawapanga
wanaume foleni lakini mimi nilikuwa na mmoja, nikiachana naye ndipo
naanzisha uhusiano na mwingine.”
KUHUSU UKIMWI
Msanii huyo alipoulizwa kuhusu orodha
hiyo ndefu ya wanaume katika zama hizi zenye magonjwa mengi, alisema
haofii maradhi yakiwemo ukimwi kwa vile anajilinda vyema.
AMZUNGUMZIA DIAMOND
Risasi: “Katika hao mastaa wakubwa Bongo yupo Diamond?”
Bozi: “Diamond
ni kijana mzuri kwa mwanamke yeyote anayejitambua lazima avutiwe naye,
kama Mungu amepanga niwe naye kimapenzi hilo halitaweza kupingika kwa
sababu ni kijana mzuri ananivutia mno, naamini ipo siku atakuwa wangu.”
Bob Junior akiwa kazini.
RISASI LAUMIZA KICHWA
Baada ya kumaliza mahojiano na Bozi,
Risasi lilikaa chini na kuanza kuumiza kichwa ili kubaini katika mastaa
hao kumi na watano ni akina nani wanaweza kuwa ndiyo walilala na msanii
huyo.
ORODHA YA GAZETI LA RISASI
Kwenye orodha ya wasanii ambao risasi
liliwaingiza kichwani kwamba wanaweza kuwa wao, si kwa tabia zao bali
kwa ukubwa wa majina yao ni Dully Sykes (Bongo Fleva), Awadh Mahsen ‘Dk.
Cheni’ (Bongo Movies), Barnaba Elias (Bongo Fleva), Jumanne Kihangala
‘Mr. Chuz’, Kiwewe, Lingo, Tito na Mboto (wote kutoka Bongo Movies).
Wengine ni Rahim Rummy Nanji ‘Bob
Junior’ (Bongo Fleva), Elibariki Emanuel ‘Nay wa Mitego’ (Bongo Fleva),
Young D, Dogo Aslay, Sam wa Ukweli na Ali Kiba (wote Bongo Fleva), Jacob
Steven (JB) (Bongo Movies), Vicent Kigosi ‘Ray’ (Bongo Movies).
Barnaba Boy.
MASTAA WASAKWA
Risasi Mchanganyiko liliamua kuwasaka
mastaa hao kwa njia ya simu ili kumuuliza kila mmoja kama anamfahamu
Bozi na kuzungumzia kama amewahi kuanguka naye.
Dk. Cheni: “Ni kweli namfahamu kuwa ni msanii wa filamu, lakini si kwa masuala ya mapenzi.”
Barnaba: “Simfahamu!
Mwanamke mwenye uhusiano na mimi ni mama Steve (mkewe) peke yake. Huyo
mnayemsema inawezekana namfahamu kikazi tu na si kimapenzi.”
Dully: “Mimi
nimeoa, nina watoto siwezi kuwa na mwanamke mwingine pembeni. Mke wangu
ananitosha, hata yeye anafahamu kuwa mimi siyo mchepukaji.”
Bob Junior: “Simjui mtu huyo.”
Sam wa Ukweli: (hakupatikana hewani).
Young D: “Simjui huyo demu.”
Dogo Aslay: “Simjui huyo mwanamke, halafu sikia, sitaki uniulize habari za huyo mtu.”
Mboto: (hakupatikana hewani).
JB: “Hilo jina hata silikumbuki kama nimewahi kulisikia.”
Ray: (hakupatikana hewani).
Mr. Chuz: “Labda namfahamu, lakini itakuwa kikazi zaidi. Tehe! Tehe!”
Kiwewe: (hakupatikana hewani).
Tito: (hakupatikana hewani).
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment