Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ enzi za uhai wake.
Stori: Waandishi Wetu Kimenuka!
Baada ya kuwepo kwa utata mkubwa juu ya kifo cha aliyekuwa mnenguaji
bei mbaya Bongo, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’, inadaiwa
kwamba waliohusika na kifo chake sasa wanasakwa kila kona.
Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni,
Dar, zilidai kwamba jeshi hilo ndilo lililozuia mazishi ya staa huyo
hadi mwili ufanyiwe uchunguzi.“Ukweli ni kwamba majibu ya kilichomuua
hayajawekwa wazi lakini wote waliokuwa naye dakika za mwisho wanasakwa
kwani kuna madai mazito kwamba alipewa kitu na watu wasiojulikana.
‘Aisha Madinda’wakati akiwa na Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka.
“Aisha alipofikishwa Mwananyamala alikuwa ameshafariki dunia. Sasa
waliokuwa naye wanajua aliyehusika kwa namna yoyote ile lazima
wakamatwe,” kilisema chanzo cha ndani cha jeshi hilo kwa sharti la
kutotajwa gazetini.
Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Camilius Wambura.
Ili kupata undani wa ishu hiyo, Jumamosi iliyopita Ijumaa Wikienda
lilizungumza na Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Camilius Wambura ambaye
alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza majibu hayajatoka hivyo ni mapema kuyazungumzia. Madai kwamba kuna mtu mmoja amekamatwa si ya kweli.”
“Kwanza majibu hayajatoka hivyo ni mapema kuyazungumzia. Madai kwamba kuna mtu mmoja amekamatwa si ya kweli.”
Aisha (35) alizikwa Ijumaa iliyopita huko Kigamboni, Dar, baada ya kukutwa na umauti wa kutatanisha Jumatano ya wiki iliyopita.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment