Baada ya kutengana na mpenzi wake safaree Samuels, Hitmaker wa nyimbo ya ‘Anaconda’ Nick Minaj ametaja vigezo vya mpenzi atakayekua naye kwa sasa.

Alisema moja ya vigezo anavyovitaka ni kupata mpenzi atakayekubali umahiri wake katika kazi zake na kuheshimu anachofanya.
“Nataka mwanaume atakayeheshimu na kuthamini uwezo wangu wa kufanya kazi.”alisema Nick Minaj.

Rapa huyo mwenye miaka 32 ameamua kuwa wazi baada ya kuvunjika kwa uhusiano wake na mpenzi wake Safaree uliodumu kwa miaka 12 na anahitaji umakini katika ufanyaji wake wa kazi.

 
Katika majibizano yake na mtangazaji Elliot Wilson alisema “Nimepoteza sehemu kubwa ya maisha yangu kwa kuachana na Safaree na sababu mojawapo nilikua busy zaidi na kazi ”
“Labda wanahitaji uangalizi zaidi na nilikua najali zaidi familia yangu,,sasa ni kazi yangu kuchagua kazi ama mapenzi.”alisema

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top