Polisi
mkoani Klimanjaro inamshikilia mzee Mungai Molel(75) kwa tuhuma za
kumbaka mtoto wa miaka 11 wa shule ya msingi Okaseni na kumjeruhi vibaya
sehemu za siri.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo Geofrey Kamwela, amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kwamba lilitokea Novemba 12 mwaka huu saa 12:00 jioni kijiji cha
Kitandu kata ya Uru Kusini.
Kamwela alisema mtuhumiwa huyo alimwita mtoto huyo nyumbani kwake na kumfanyia kitendo hicho cha kikatili.
“Alimwita
nyumbani kwake na kumbaka kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali
sehemu za siri na kusababisha mtoto huyo kulazwa katika Hospitali ya
KCMC” alisema Kamwela.
Kamanda
Kamwela alisema mtoto huyo yupo katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa
matibabu kutokana na kuharibika vibaya sehemu za siri .
Alisema
mzee huyo alimbaka kwa nguvu mtoto huyo hali iliyomsababisha mtoto
kupiga makelele na kuokolewa na majirani wa mzee huyo na kutoa taarifa
polisi kutokana na kwamba walimkuta mtoto huyo akivuja damu nyingi.
Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na kwamba atafikishwa mahamani upelelezi utakapo kamilika.
Aidha
Kamanda Kamwela aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la
Polisi nchini katika kufichua matukio mbalimbali ya kihalifu ili kuweza
kunusuru maisha ya wananchi na mali zao, huku akiahidi jeshi kuendeleza
ushirikiano huo.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Related Posts
- HATIMAYE KINACHOWAUA WASANII KWA KASI CHAJULIKANA!! SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI..25 Dec 20140
MWAKA 2014 unakatika, matukio ya kukumbukwa ni pamoja na wasanii Bongo kupoteza maisha katika maz...SOMA ZAIDI»
- PICHAZ: MTUMZIMA SUPER STAR SINGER PATCHO MWAMBA ALA KIPIGO CHA MBWA MWIZI KWA KUBAMBWA NA MKE WA MTU!!25 Dec 20140
Picha kwa hisani ya @selfielife instagram Inasemekana kuwa mwigizaji na mwanamuziki wa Dan...SOMA ZAIDI»
- TABIA ZA MSICHANA ANAYEPENDA LAKINI HAWEZI KUSEMA NI HIZI HAPA.23 Dec 20140
1. Atakutega kupata attention yako. Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda au l...SOMA ZAIDI»
- NJIA YA KUPATA MTOTO WAKIKE AMA WAKIUME NI HII HAPA23 Dec 20140
Ni vipi jinsia ya mtoto huainishwa?Kinyume na wengi wanavyofikiria kwamba mwanamke au mwil...SOMA ZAIDI»
- WATOTO WA KIKE NA MAPENZI YA HARAKA HARAKA- WAKINA MAMA JE MNAWAELIMISHAJE NA KUWAKUZA WATOTO WA KIKE ILI KUWAANDAA KUPAMBANA NA MAISHA YA KIMAPENZI?23 Dec 20140
Hivi ni mimi tuu bado niku nyuma ama ndo kuamka kwa tamaduni zetu za kiafrika? Siku hiz...SOMA ZAIDI»
- MWALIMU ANYONGA MTOTO GESTI,MWILI WAHIFADHIWA KWENYE KORIDO HOSPITALI HAINA MOCHWARI21 Dec 20140
Askari wa jeshi la polisi wakiwa eneo la hospitali ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Mwili w...SOMA ZAIDI»
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.