
Ripota wa bekamtanzania.com
Elisa Shunda kutoka Dar es salaam ameziwasilisha hizi picha za wakazi
wa kata ya Ubungo wakiwa katika msururu wakisubiri kupatiwa vitambulisho
vyao vya uraia ambavyo vimekuwa ngumu kuvipata kutokana na mpangilio
unaolalamikiwa kuwa mbovu wa mamlaka ya vitambulisho (NIDA).
Baadhi ya wananchi waliofika katika kituo hicho na vingine wamekuwa
wakilalamika kutokuona majina yao katika picha na majina yanayobandikwa
katika ukuta wa ofisi za mitaa na kata.

Wengine
wanasema wafanyakazi wa Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA)
wamekuwa wakiwasaidia watu wengine kuwapatia vitambulisho kinyume na
utaratibu jambo ambalo huwa linaleta msongamano mkubwa sana na kuwafanya
wafanyakazi hao wasifanye kazi zao kwa ufanisi.

Baadhi
ya wananchi waliofika katika kituo hicho wakijaribu kuangalia majina
yao kama yapo au hayapo ambapo katika kituo kingine baadhi yao
walisemahawakuona majina yao japokuwa walijiandikisha katika kituo
hicho.

Wananchi
wakihangaika kuingia ndani kupatiwa vitambulisho vyao baada ya kuona
msafara hauendi na kuna watu wanaingia ndani bila utaratibu maaalumu

Afisa
wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) akiita majina kwa pembeni
ili kurahisisha watu waondoke mapema ila bado wananchi wamelalamikia
utaratibu mbovu wa ugawaji wa vitambulisho.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.