Kama haukusikiliza ama kutazama Kikao
cha Bunge Dodoma leo, moja ya masuala yaliyotawala ni kuhusu Mamlaka ya
Bunge na Mahakama, wa kwanza kuzungumza alikuwa David Kafulila; “…
Naomba mwongozo kuhusiana na taarifa ya PAC kuhusiana na sakata la
ufisadi wa ESCROW kama italetwa ama haitaletwa na msingi wa swali lile
ulikuwa ukizingatia kwamba zimekuwepo taarifa za mkakati wa kuhakikisha
Mahakama inatumika kuhakikisha ripoti ile hailetwi Bungeni na kufikia
mwisho…”
“…. Kwa
kuwa suala hili ni suala nyeti, Watanzania wote wanafuatilia jambo hili
kwa umakini kujua hatma ya jambo hili naomba Mheshimiwa naibu Spika
utupatie mwongozo wa Bunge na Watanzania kuhusu uhakika wa Ripoti hii
kuletwa Bunge hili ili kuondoa mashaka ambayo yamekuwa yakijengeka
kwamba kuna mikakati.. kuna njama ambazo Mahakama inataka kutumika kama
kichaka cha kuweza kuficha wezi wa hizi fedha, na kwa hiyo Watanzania..
ili kusudi Watanzania waliamini Bunge lako tukufu kwamba ndiyo ‘Supreme
organ’ kwenye uendeshaji wa nchi hii na kwamba jambo hili litajadiliwa
katika Bunge hili na tutafanya maamuzi ya mwisho…“– David Kafulila.
“…Lakini
vilevile Watanzania wafahamu kwamba sio tu kwamba Mahakama haipaswi
kuingiliwa na Bunge lakini pia Mahakama haipaswi kuingilia Bunge.
Ningeomba uhakikishie Watanzania kuhusiana na jambo hili kwa sababu
majibu ya Waziri Mkuu yalikuwa nusunusu hayatoi uhakika kwamba Ripoti
hii italetwa au haitaletwa…”– Kafulila.
Naibu Spika Job Ndugai akajibu; “… Asante sana, nitatolea mwongozo jambo hili mwishoni…”
Baada ya hapo akateuliwa Mbunge Esther
Bulaya, ambapo kutokana na mwongozo alioutoa ulikuwa sawa na wa Mbunge
Kafulila akaombwa asubiri ili wachangie wengine, mwongozo kuhusu ESCROW
ungehitimishwa mwisho wa kikao hicho.
Naye Moses Machali alipewa nafasi, akasema haya; “…
Ukifanya ‘situational analysis’ ya mwenendo wa Bunge letu hivi sasa,
Bunge limegubikwa na kupuuzwa na kudharauliwa na mihimili mingine
ikiwemo Serikali na sasa Mahakama nayo imeanza ku-penetrate kwenye
kudharau hili Bunge…”
“… Suala
langu ni nini.. Unadhani Wabunge ambao pengine tungependa kuona haki,
kinga na madaraka ya Bunge hayaporwi, tufanye nini au tutumie nguvu gani
za ziada ili kuweza kudhibiti Mihimili mingine ambayo imekuwa inataka
kupora uhuru na Madaraka ya Bunge kama ambavyo imeainishwa kwenye Ibara
ya 100… kama hili suala ambalo ESCROW leo hii linatikisa…”– Machali
Kama hukupata nafasi ya kusikiliza mjadala huo wa Bunge Leo Novemba 20 unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play hapa.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Related Posts
- HATIMAYE KINACHOWAUA WASANII KWA KASI CHAJULIKANA!! SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI..25 Dec 20140
MWAKA 2014 unakatika, matukio ya kukumbukwa ni pamoja na wasanii Bongo kupoteza maisha katika maz...SOMA ZAIDI»
- PICHAZ: MTUMZIMA SUPER STAR SINGER PATCHO MWAMBA ALA KIPIGO CHA MBWA MWIZI KWA KUBAMBWA NA MKE WA MTU!!25 Dec 20140
Picha kwa hisani ya @selfielife instagram Inasemekana kuwa mwigizaji na mwanamuziki wa Dan...SOMA ZAIDI»
- TABIA ZA MSICHANA ANAYEPENDA LAKINI HAWEZI KUSEMA NI HIZI HAPA.23 Dec 20140
1. Atakutega kupata attention yako. Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda au l...SOMA ZAIDI»
- NJIA YA KUPATA MTOTO WAKIKE AMA WAKIUME NI HII HAPA23 Dec 20140
Ni vipi jinsia ya mtoto huainishwa?Kinyume na wengi wanavyofikiria kwamba mwanamke au mwil...SOMA ZAIDI»
- WATOTO WA KIKE NA MAPENZI YA HARAKA HARAKA- WAKINA MAMA JE MNAWAELIMISHAJE NA KUWAKUZA WATOTO WA KIKE ILI KUWAANDAA KUPAMBANA NA MAISHA YA KIMAPENZI?23 Dec 20140
Hivi ni mimi tuu bado niku nyuma ama ndo kuamka kwa tamaduni zetu za kiafrika? Siku hiz...SOMA ZAIDI»
- MWALIMU ANYONGA MTOTO GESTI,MWILI WAHIFADHIWA KWENYE KORIDO HOSPITALI HAINA MOCHWARI21 Dec 20140
Askari wa jeshi la polisi wakiwa eneo la hospitali ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Mwili w...SOMA ZAIDI»
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.