Kwa taarifa zilizotoka kwa uongozi wa kituo hicho siku kadhaa zilizopita ni kwamba wanapanga utaratibu maalumu na watazisajili bajaji 20 tu ambazo zitaruhusiwa kuingia ndani.
Ni kituo kipya cha Mabasi ambacho kimechukua nafasi ya kile kidogo cha Ubungo kilichokuwepo karibu na TANESCO, hiki kipya kilichopo Sinza kilianza kufanya kazi October 23 2014.
Baadhi
ya madereva wa bajaji wakiwa wameegesha bajaji zao nje huku wakiwa
wanajadili hatima yao itakuwaje jinsi ya kubeba abiria katika kituo
hiko.
Wengi wa abiria walikuwa wanalalamika kutokana na mabasi mengi kutokufika katika eneo hilo hivyo usafiri ulikuwa mgumu.
Taa
za kituo cha mabasi Sinza ambazo zinawaka kwa kutumia nguvu ya Jua,
baadhi ya watu ambao huwa maeneo hayo usiku wanasema ikifika saa tano
usiku huwa zinazima, kituo cha polisi kina umeme wa tanesco.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment