Staa
 wa Filamu za Kibongo, Yvonne Sherry ‘Monalisa’ hivi karibuni aliweka 
wazi kuwa anatamani kuolewa lakini hajampata wa kumuoa.Monalisa 
alifunguka maneno hayo baada ya uvumi kuenea kuwa amepata mtu anataka 
kumuoa na mipango ya ndoa iko tayari.
“Mh!
 Wewe si wa kwanza kuniambia maneno haya jamani hivi yanatoka wapi? Mimi
 sijapata mtu wa kunioa jamani ila nikimpata nitaolewa kwa sababu jua 
limekuchwa pia ndoa ni jambo la heri,” alisema Monalisa
Katikati
 ya mwaka huu, Monalisa alionyesha matamanio yake ya ndoa ambapo alivaa 
shera kwenye harusi ya rafiki yake na kuingia na mumewe ikiwa kama 
maigizo kituko hicho kiliipendezesha shughuli hiyo
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
 

Post a Comment