Mwanamke mmoja amenusurika kuuwawa
kutokana na kupigwa na mume wake ambaye ni askari, kisa ikiwa ni
mwanamke huyo kushindwa kumnunulia vocha.
Akisimulia mkasa huo uliotokea Uganda, mke wa askari huyo Eva Okoth amesema
mume wake alikuwa ametoka kunywa pombe na rafiki zake, akaanza
kujisikia vibaya baada ya kushindwa kula na kutapika akihisi rafiki zake
walimwekea sumu katika pombe, hivyo akampatia hela mke wake ili
akanunue vocha kuwapigia ndugu zake ili awaage kwamba anakufa.
Mwanamke
huyo anasema wakati huo ilikuwa saa 11 alfajiri, maduka yalikuwa
hayajafunguliwa, askari huyo alichukua bunduki na kuanza kufyatua risasi
huku akitishia kumuua na kujiua yeye.
Eva alikimbia kujificha jikoni, taarifa kutoka kwa msemaji wa kituo cha Polisi Lameck Kigozi amemtambua askari huyo kuwa ni John Okoth
na kueleza kuwa baada ya askari wenzake kusikia milio ya risasi
walikimbilia katika nyumba ya askari huyo na alipowaona aliendelea
kuwarushia risasi japo hakuna aliyedhurika.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment