Taarifa iliyonifikia muda mfupi uliopita inahusu ajali ya kuanguka kwa Jengo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa.
Mtu mmoja amefariki na wafanyakazi na
wakazi wengine wa eneo la Ruaraka, Kenya wamenusurika kifo kutokana na
ajali ya kuanguka kwa jengo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa, kwa
mujibu wa mashuhuda wanasema ajali hiyo imesababishwa na nyufa
zilizokuwa katika jengo hilo.
Taarifa ya Citizen News
imesema wakazi wa eneo hilo wamesema kwamba waliwahi kuwakemea wamiliki
wa jengo hilo kwa kufanya ujenzi chini ya kiwango lakini hakuna
mabadiliko yaliyowahi kufanyika.
Uchunguzi unafanyika kubaini sababu iliyopelekea ajali hiyo.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment