Dustan Shekidele, Morogoro
JAMAA aliyetajwa kwa jina moja la Aziz, amenusa kifo laivu baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kisha kukamatwa akituhumiwa kwa wizi wa pikipiki almaarufu bodaboda Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, jamaa alikamatwa hivi karibuni usiku mnene akidaiwa kutaka kutekeleza uhalifu huo jirani na Kumbi za Starehe za Nyumbani Park na Samaki Sports zilizopo maeneo ya Kihonda mjini hapa.
Aziz ‘akitaitiwa’ baada ya kutaka kuiba Bodaboda.
Mwanahabari wetu, akiwa ndani ya moja ya kumbi hizo alitonywa kwamba nje Aziz alikuwa ‘ametaitiwa’ baada ya kunaswa akijaribu kuiba moja ya bodaboda zilizokuwa zimeegeshwa nje.
Ilidaiwa kwamba mabaunsa wa eneo hilo ndiyo waliomshtukia jamaa huyo ambapo raia wenye hasira kali walipomsachi walimkuta na hirizi hivyo wakataka kumuua kwa kipigo kikali kilichosababisha kuloa damu tepetepe ndani ya dakika sifuri.

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top