Watoto wadogo wamekuwa katika hatari
ambapo mara nyingi tumesikia taarifa za watoto kufanyiwa vitendo
mbalimbali vya kikatili na watu wazima.
Taarifa kutoka katika mitandao ya
Nigeria imesema watoto wadogo wawili ndugu, mmoja mwenye umri wa miaka
sita na mwingine miaka nane wamebakwa na mwanaume ambaye amewahi kuwa na
mahusiano na mama yao.
Mtu huyo, Terkula Iorpuur
mwenye miaka 32 aliyekuwa akijishughulisha na kazi za ujenzi,
aliripotiwa kituo cha Polisi cha ‘B’ Division Police Station na mjomba
wa watoto hao ambapo alikamatwa.
Mama wa watoto hao aligundua hali ya utofauti kwa watoto hao ambapo walikuwa hawatembei vizuri.
Mwendesha mashtaka Terzungwe Kajo amesema uchunguzi umeonyesha mshtakiwa huyo ana maamukizi ya VVU.
Kesi hiyo imesogezwa mbele mpaka tarehe 4 Desemba ambapo itatajwa tena na mshtakiwa amerudishwa gerezani.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment