Alilazwa akiwa na dalili za homa kali, manjano, kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili ambapo alilazwa kwenye Kituo cha Afya Mwangika tarehe 15 hadi 16 Oktoba 2014 kabla ya kuhamishiwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema October 17 na kufariki duniani siku hiyohiyo saa 3.30 usiku.
Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na historia ya kusafiri kwenda nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola na hakuwahi kupokea mgeni kutoka nchi hizo ndani ya siku ya 21 zilizopita ambapo alizikwa kama mgonjwa wa Ebola na hakukuwa na ndugu wala yeyote asiehusika isipokua Watu maalum waliokua wamevalia mavazi ya kujikinga.
Baada ya hapo Sampuli ya damu ya mgonjwa kwa ajili ya uchunguzi wa Kimaabara ilichukuliwa ili ithibitike ni ugonjwa gani umemuua sababu serikali iliahidi kutoa majibu hayo.
November 14 2014
‘Yule binti wa miaka 17 alieumwa mpaka akafariki alikua ana ugonjwa wa ini ambapo Wataalamu wanatuambia upande wa Afya kwamba mgonjwa wa Ini anapofikia hatua flani anaweza kupata dalili flani ambazo mtu anaweza kufikiria ni Ebola, tulijitahidi kuhakikisha kwamba hizo sampuli zimepelekwa kwenye Maabara Dar es salaam na taarifa tulizozipata ni kwamba hakuna kabisa dalili za ugonjwa wa Ebola kwa yule mgonjwa ambae alifariki‘ alisema mkuu wa wilaya ya sengerema
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment