Majeruhi mwingine
majeruhi
Baadhi
ya majeruhi waliolipukiwa na baruti jana wakati wakivua samaki kwa
kutumia baruti katika Kisiwa cha Karange tarafa ya Pongwe wakiwa
wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza
baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikonoPicha na Elizabeth Kilindi.
Wakazi
wawili wa kata ya Tangasisi tarafa ya Pongwe wilayani Tanga
wamejeruhiwa vibaya viungo mbalimbali vya mwili kwa kulipukiwa na baruti
wakati wakivua kwa kutumia dhana za uvuvi haramu kwenye kisiwa cha
Karange.
Tukio
hilo limetokea mnamo Novemba 12 mwaka huu majira ya saa nane mchana
katika kisiwa ambapo majeruhi hao wakiwa kwenye ngalawa yenye namab za
usajili TTA 315 wakati wakijianda kutegesha baruti hizo ndipo
zilipowalipukia.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Tanga Freisse Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuwataja majeruhi hao kuwa ni Hamis Omari ambaye amekatika mkono
wa kulia na ameumia jicho la kulia,huku majeruhi mwingine Adamu
Selemani amekatika mikono yote miwili, pamoja na kupoteza macho yote
mawili.
“Hali
ya majeruhi wote wawili ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya
bombo ni mbaya hii inaonyesha ni kwa kiasi gani uvuvi haramu ulivyo na
madhara makubwa kwa jamii pamoja na viumbe wa baharini “alisema Kamanda
Kashai.
Hata
hivyo kamanda Kashai alitumia fursha hiyo kuwa taka wakazi wanaoishi
maeneo ya bahari kutoa taarifa ya wavuvi wanaojihusisha na uvuvi haramu
ili kuweza kuwachukulia hatua mapema kabla ya kutokea kwa madhara zaidi.
NA ELIZABETH KILINDI, TANGA
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment