Kuhusu vita dhidi ya biashara haramu ya meno ya tembo, mataifa mbalimbali yamekuwa yakikemea biashara hiyo lakini bado wapo watu ambao wameendelea kuifanya.
Maafisa Wanyamapori watano
wamesimamishwa kazi ili kupisha upelelezi kufanyika kufuatia kupotea kwa
meno ya tembo kwenye mazingira ya kutatanisha yakiwa katika sehemu ya
ulinzi mkali wa Serikali, Uganda.
Akizungumza na AFP
mkurugenzi wa Uganda Wildlife Authority, Raymond Engena amesema wameomba
msaada wa Kikosi cha Askari wa Kimataifa (Interpol) kufanya upelelezi
kufuatia agizo la Rais Museveni la kutaka wahusika wote kukamatwa kutokana na upotevu huo.
Meno hayo yana uzito wa kilo 1,335 yana
thamani ya Dola Mil. 1.1 za Uganda ambapo imesemekana baadhi ya maofisa
hao wamekuwa wakiyachukua meno hayo kwa ajili ya kutumia kuwatega
wafanyabiashara wa meno hayo lakini hawayarudishi baada ya kuyafanyia
kazi hiyo.
Ripoti zinaonyesha idadi ya tembo 35,000
wamekuwa wakiuawa Afrika kila mwaka kutokana na biashara hiyo kuonekana
kuwa na soko kubwa nchi za Asia.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment