kimemnasa msaidizi wa kazi za ndani (hausigeli) akifanya biashara haramu ya kuuza mwili kwa kisingizio cha mshahara kiduchu.
Kushoto ni hausigeli akifanya biashara ya uchangudoa maeneo ya
Sinza jijini Dar.Tukio hilo la aina yake liliingia kwenye kamera za OFM
maeneo ya Sinza jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo msichana
huyo wa kazi alikutwa kwenye harakati za kusaka wanaume ili kuwapa penzi
kwa malipo. Mara baada ya kumnasa na kumlamba picha akiwa na wenzake
ambao nao kama yeye walikuwa wamevaa nguo fupi yaani nusu utupu, alianza
kuangua kilio hasa alipokuwa akihojiwa kwa nini anajihusisha na
biashara hiyo hatarishi katika maisha yake.
“Jamani mmenipiga picha mtanipotezea kazi yangu, jamani mimi
nimeajiriwa, ni mfanyakazi wa ndani kwa mheshimiwa Mikocheni (Dar),
nafanya kazi za ndani hii yote ni kujitafutia riziki nje ya kazi,”
alilalama binti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi
23.
Baadhi ya machangudoa wakiwa mawindoni.Binti huyo aliwaambia OFM
kwamba alifikia hatua hiyo ya kujiingiza katika biashara hiyo ya ngono
kutokana na ugumu wa maisha huku lawama akizielekeza kwenye mshahara
kidogo wa kazi za ndani.
“Mshahara wangu ni mdogo sana, nalipwa shilingi elfu 50 kwa mwezi,
nina watoto wawili kijijini hivyo hautoshi. Kama vipi nitafutieni kazi
nitaacha kuuza mwili,” alisema.
Alipoulizwa namna anavyotoka kwa bosi wake kwenda kujiuza, hausigeli
huyo alisema kwamba huwa anakula dili na walinzi wa bosi wake usiku
wakiwa wamelala anatoka na akirudi freshi anawakatia walinzi chao.
Machangudoa wengine wakizikimbia kamera.Alisema kuwa yeye analala
katika vyumba vya uani kwa hiyo anapotoka waajiri wake hao inakuwa
vigumu kumsikia kwani wanakuwa wamepitiwa na usingizi.
Aliendelea kueleza kwamba kuna siku nyingine huwa anarudi nyumbani akiwa amevuna fedha nyingi kuliko mshahara wake.
“Hii kazi yangu inaniingizia kipato kikubwa sana kuliko mshahara,” alisema hausigeli huyo.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment