Na Imelda Mtema
Prizenta wa Kituo cha Radio E-FM cha jijini
Dar, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ anadaiwa kukumbwa na mauzauza
yaliyodaiwa ni mapepo na kujikuta akipiga makelele barabarani.
Prizenta wa Kituo cha Radio E-FM cha jijini Dar, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’.
Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilidai kwamba, ishu hiyo ilijiri
maeneo ya Makongo jijini Dar es Salaam, juzikati wakati staa huyo
akielekea msibani ambapo rafiki yake kipenzi aitwaye Skitter alifariki
dunia.
Chanzo hicho kilidai kwamba Penny alikuwa akiendesha gari kwa mwendo
wa kawaida, alipofika maeneo hayo aliegesha gari pembeni na kuanza
kupiga kelele akilia kwa uchungu hivyo kuwaacha watu waliomshuhudia
wakiwa midomo wazi wakitaka kujua kilichompata mtangazaji huyo.
Mpashaji
wetu huyo alizidi kueleza kwamba baada ya kama dakika kumi, Penny
aliondoa gari na kuendelea na safari.
Paparazi wetu aliponyetishiwa ishu hiyo alimtafuta Penny na kumuuliza
kuhusu tukio hilo ambapo alisema alikuwa akienda kwenye msiba wa rafiki
yake, alipokaribia kufika alipata uchungu ndiyo akatokewa na hali hiyo.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment