Kumekuwa
na taarifa kuhusu kuwepo migogoro mbalimbali inayohusisha Wabunge
wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki ambapo Mbunge
Shy-Rose Bhanji amehusishwa sana kwenye vichwa vya habari.
Kwenye kikao cha Bunge November 20 2014 Dodoma Hatibu ambae ni mbunge wa Zanzibar aliuliza >>> “…
Sisi wabunge wa bunge hili ndiyo wapiga kura wa kuwachagua wawakilishi
wetu wa kutuwakilisha katika bunge la Afrika Mashariki, kumekuwa na
taarifa za kulipaka Taifa hili matope kulitia aibu kutokana na baadhi
ya wawakilishi wetu, Wabunge wetu wa Afrika Mashariki kutokana na
matendo wanayoyafanya kule..”
“…Ni
lini hasa kinachoendelea pale na hatua gani zilizochukuliwa kuhusu
ukosefu wa nidhamu uliojitokeza kwa mbunge Shyrose Banji wazi wazi na
bili hali hakuna taarifa yoyote, Mheshimiwa Naibu Spika naomba mwongozo
wako…”– Hatibu.
Baada ya swali waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akawasha kipaza sauti na kutoa haya majibu “…Naomba
nitoe taarifa kwamba kinachotokea katika Bunge la Afrika Mashariki kwa
kiasi kikubwa kinahusu mgogoro wa spika mwenyewe, hilo ndiyo chanzo cha
matatizo mengi, kwa hiyo wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki
wamegawika kataka makundi mawili, kuna kundi linalotaka Spika lazma
aondolewe, na wengine wanadai wanamtetea abaki…”
..Sasa
katika kundi ambalo wanataka abaki imeonekana Tanzania ndio kikwazo,
kwa sababu ili upate uamuzi ndani la Bunge la Afrika Mashariki katika
suala lolote lazima upate akidi inayotosheleza kutoka kila nchi, sasa
wabunge wa Tanzania ambao mwanzoni waliunga mkono hoja ya kumuondoa yule
Spika wamefuta hilo na wamekubaliana aendelee kwa hiyo imeleta chuku
kiasi Fulani…“– Sitta.
“…Katika
tukio ambalo limetokea juzi na nasema hivi kwa sababu Naibu Waziri
wangu yuko kule kwa hiyo ni jambo halisi, kilichotokea sio kama
kinavyoelezwa Mheshimiwa Shyrose Banji ambaye anahesabika ni mfuasi
mkubwa wa Yule Spika kiasi kwamba wenzie wanamuona kama kibaraka vile,
alikuwa anapita katikati ya Wabunge wengine kuwahi usafiri kwa bahati
mbaya akamgonga Mheshimiwa Ndelakindo Kessy, Mheshimiwa Ndelakindo
akahamaki na kwa kusaidiwa na baadhi ya Wabunge wengine wa Uganda
akaenda kituo cha Polisi kutoa taarifa kwa madai kwamba amefanyiwa
makosa ya jinai wanaita ‘assaults’…“– Sitta.
“
“>…Ikabidi aitwe ‘Sergeant at Arms’ wa Bunge la EALA ambaye
alikwishaanza jitihada za kulifanya jambo lile liishie ndani ya Bunge na
katika jitihada hizo alifika mbali kidogo akawezesha Wabunge wetu hao
wawili waweze kusikilizana na ninavyotoa taarifa hivi sasa ni kwamba
jana suala hili limekwisha na haliendelezwi na Polisi tena…
“– Sitta.
Hivi ndivyo Waziri Sitta alimalizia kujibu suala hilo; “…Sasa
yale mengine yaliyosema kwamba alifanya mambo ya hovyo Mheshimiwa yule
tena kama miezi miwili iliyopita, bado yako mikononi mwa tume ya Bunge
la Afrika Mashariki hadi hapo watakapolishughulikia hatuwezi kufanya
kitu chochote, na tukishapata taarifa ya tume ya Bunge la Afrika
Mashariki basi mimi nitatoa taarifa kwa Mheshimiwa Spika ili sasa sisi
kwa wote kama jimbo la uchaguzi La Wabunge hao tuone ukweli ni upi na
tujue hatua ya kuchukua..”– Sitta.
Kama ukihitaji kusikiliza maswali na majibu hayo kutoka kwenye kikao cha bunge, bonyeza play hapa.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment