Mbunge wa Ileje Aliko Kibona ndio aliuliza swali bungeni akiwa na lengo la kutaka kujibiwa na Wizara ya michezo kuhusu
sheria kwamba kila mwajiri ahahakikishe anapomlipa mfanyakazi wake bila
kujali aina ya mkataba, anamuwekea pesa katika mifuko ya hifadhi ya
jamii.. akijumlishia pia na club za soka Tanzania ziweze kuombwa
kuangalia uwezekano kuwekea hifadhi ya jamii wachezaji wake.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia akawasha vipaza sauti na kusema haya >>> “Tutashirikiana
na SSRA kuangalia namna gani sasa tuweze kuzishawishi club zetu ili
wachezaji wao waweze kuingia katika mifuko hii.. lakini pia nitumie
fursa hii kuipongeza sana klabu ya Yanga kupitia mwenyekiti wake Yusuph
Manji.. Yanga tayari wameshazungumza na NSSF na wachezaji wao wote
sasa wanapewa mikopo ya nyumba, hii ni hatua moja nzuri na sisi kwa
upande wetu tutatumia fursa yetu kuzungumza na club nyingine ili
wachezaji wao na waweze kufanya hivyo, hata wale wa Simba…”
Mheshimiwa Ismail Aden Rage alimalizia kwa kujibu hivi; “… Kwa taarifa tu kwa bunge lako tukufu, Simba wanaujenga uwanja wao wa kisasa kule Bunju na watajenga nyumba kwa wachezaji wao…”
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment