.
Kwenye hii picha ya kwanza inaonekana sehemu ya kupaki pikipiki aina
ya Bajaji ambapo kibao chake kimezibwa kuzuia bajaji zisiingie ndani,
kwenye siku ya kwanza bajaji zilikuwa zinaingia ndani na kulipa sh.500
kila wakitoka na abiria ila ilipofika mida ya mchana walikatazwa kuingia
ndani.
Kwa taarifa zilizotoka kwa uongozi wa kituo hicho siku kadhaa
zilizopita ni kwamba wanapanga utaratibu maalumu na watazisajili bajaji
20 tu ambazo zitaruhusiwa kuingia ndani.
Ni kituo kipya cha Mabasi ambacho kimechukua nafasi ya kile kidogo
cha Ubungo kilichokuwepo karibu na TANESCO, hiki kipya kilichopo Sinza
kilianza kufanya kazi October 23 2014.
Baadhi
ya madereva wa bajaji wakiwa wameegesha bajaji zao nje huku wakiwa
wanajadili hatima yao itakuwaje jinsi ya kubeba abiria katika kituo
hiko.
Wengi wa abiria walikuwa wanalalamika kutokana na mabasi mengi kutokufika katika eneo hilo hivyo usafiri ulikuwa mgumu.
Hiki ni kituo kipya cha polisi kilichopo ndani ya stand hii.
Askari wa usalama barabarani wakiwa kazini ndani ya kituo hiki kipya
Taa
za kituo cha mabasi Sinza ambazo zinawaka kwa kutumia nguvu ya Jua,
baadhi ya watu ambao huwa maeneo hayo usiku wanasema ikifika saa tano
usiku huwa zinazima, kituo cha polisi kina umeme wa tanesco.
Post a Comment