Zoezi la utoaji wa Vitambulisho vya
Uraia limeendelea leo, kituo cha Televisheni TBC1 kimeripoti kuhusu
namna zoezi hilo lilivyofanyika.
Katika taarifa hiyo baadhi ya watu waliohojiwa maeneo ya Sinza wameongelea kuhusu hilo, mmoja wa watu hao Chiku Abdalla amesema; “….Utaratibu
ni mbovu, kwa hiyo kwa mtazamo wangu mimi kama mimi..wangefanya
utaratibu kwamba Sinza C wachukulie Serikali ya mtaa C, D, E na A… yaani
kila mtaa ukachukulie kwenye Serikali yake ya mtaa…”
Naye Abbas Mohamed amesema; “..Sasa
zoezi lirudi Serikali za mtaa sio kata kama hawana vifaa waongezewe
vifaa… Halafu mimi nauliza, kitambulisho kina miaka kumi, ina maana mimi
uraia wangu miaka kumi…”
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Sinza ‘A’ na Sinza ‘B’, Ibrahim Mabewa amesema; “…
Kwenye kata kama hizi ambazo zina changamoto ni vizuri wakarudisha
mpaka kule kwenye mitaa.. ili kila mmoja akawajibike kwenye mtaa wake..
naamini inaweza ikapunguza hizi changamoto za vurugu na mambo haya,
vinginevyo tuhuma za wananchi haziwezi kuisha..”
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment