Wana mmu mwenzenu leo ninalo hili,wimbi la matukio ya wanaume wengi ambao kutwa hawaishi kulalamika kuwa wanapigwa mizinga na wake au wapenzi wao limezidi kuongezeka.

Jamani ukweli ni kwamba ukikuta wewe ni mwanaume na una umia sana kumpa mkeo au mpenzio pesa kwa kupenda au hata kwa kuombwa huenda ukawa na matatizo haya matatu au mojawapo:

1.hujui jukumu lako au daraka lako kama mwanaume,:
kwani kiasili mwanaume alipewa jukumu la kumtunza mke wake na ndio maana mwanaume aliambiwa atakula kwa jasho na si mwanamke kwa hiyo wewe kama mwanaume huna budi kumtunza mkeo kwa kila kitu tena bila malalamishi.


2.huna mapenzi na huyo mkeo au mpenzio:
Jamani kiukweli ukimpenda mtu unawiwa kumfanyia mambo mazuri yaani huoni haja ya umpendaye kuteseka ilhali wewe upon na uwezo wa kumsaidia upo,kwa hiyo ukijikuta unalalamika unapigwa mizinga wakati mpenzio anakuomba hata pesa ya mtaji labda au hata ana shida Fulani ya pesa jua huna mapenzi naye,pengine umelzimishwa kuwa naye au kuna hali zimekulazimu kuwa naye au umekuwa naye tu kwa sababu wote uliokuwa unawataka hakuna hata mmoja aliyekukubali ila huyo kwa hiyo unahisi hasira kumhudumia unaona mzigo mkubwa mno.


3.huna feature naye (mpenzi,mchumba)
Uko naye kwa ajili ya kupoteza muda huna malengo naye kwa hapo baadaye,yaani you hit and run na kwa hivyo swala la kumhudumia au kumpa pesa kwako ni kero na shida tupu.


Mwanaume kuhudumia bwanah,hivi huoni raha kujua kuwa unayategemeza maisha ya umpendaye,hujisikii vizuri?hujioni mwanaume wa shoka?


N:B siongelei wale wanawake wenye tabia za waziwazi za kuchuna wanaume nawaongelea wanaume ambao hawapendi na wanaona ni usumbufu kuwahudumia wake au wapenzi wao au hata wanatamani wake au wapenzi wao wawe na kazi pia ili waweze kujihudumia wao wenyewe.maanake kuna wanaume wengine analalamika live kabisa kwa wenzie nyie jamani mi mke wangu/mpenzi wangu anaomba hela huyo au yaani ye kila siku kuomba omba t tu hivi anajua uchungu wa kutafuta hela huyu?

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top