BAADA ya hivi karibuni Msanii wa Filamu na Muziki Bongo, Baby Madaha kusema ameamua kuwapanga wanaume, hivi sasa ameibuka na jipya na kudai kwamba huwa hatumii kinga ‘kondom’ hata siku moja.

Akipiga stori na paparazi wetu, Baby Madaha alisema kabla hajaanguka penzini na mwanaume lazima akapime kwanza Ukimwi na baada ya hapo ndipo mambo mengine yanaendelea hivyo akishahakikisha huyo mwanaume ni mzima huwa ahangaiki kutumia kinga.

“Japokuwa nawapanga wanaume lakini najali sana afya yangu yaani kila baada ya miezi mitatu huwa naenda kupima kabla sijaingia naye kwenye uhusiano, nikikuta yuko fresh tunaendelea na mapenzi yetu na huwa situmii kinga kwa sababu nakuwa nimeshajua afya yake.

Ikitokea amenizingua nampiga chini namchukua mwingine naenda kumpima hivyohivyo maisha yanasonga mbele,” alisema Baby Madaha.

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top