STAA wa filamu Bongo ambaye miezi michache iliyopita
alifunga pingu za maisha na mwanaume mwenye asili ya Denmark, Lucy
Komba amekwea pipa kuelekea nchini humo kwenda kuishi na mumewe sambamba
na kumpelekea mwanaye amlee.
Akipiga stori na paparazi wetu kupitia Mtandao wa WhatsApp akiwa
nchini Denmark, Lucy alisema aliamua kuondoka kimyakimya na kumfuata
mumewe kwa kuwa alimisi mambo mengi kwake, pia suala la ndoa
halimuhitaji aishi mbali na mumewe na kwa kuwa mwanaume huyo anampenda
sana mtoto wake japo hajazaa naye ndiyo maana akaamua kuondoka naye
akamlee.
“Najua mtu anaweza kuongea vyovyote, mimi nilimmisi mume wangu na
mwanangu naye alitamani sana kuja kumsalimia baba yake ndiyo maana
nikamleta huku amlee ila baadaye atarejea Bongo,” alisema Lucy.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment