Nguvu ya mitandao ya kijamii ni kubwa
sio tu iliweza kusababisha mtu akajivuta taji la U-Miss bali hadi kuwapa
ushidi kina Diamond na Idris..sasa sijui hii ya hii picha ya Jambazi la
Bongo Movie ingetupeleka wapi.
Picha hii inasambaa kwa kasi sana
mitandaoni, imuonyesha jambazi akimuonyesha bastola mwandada (ambae bila
shaka anaonekana mwigizaji Irene Uwoya). Sasa cha kishangaza wengi ni
kwamba “kaka jambazi” amevua viatu!!!!!. Hii imepelekea watu wengi
kuiponda sana tasnia ya filamu hapa nchini kuwa hawako “ serious” na
kazi yao.
Hii imemfanya mwigizaji Jackline Masawe "Wolper" kutolea ufafanuzi, na hivi ndivyo alivyofunguka;
“Nimeona watu wengi wanapost hii pcha jamani hii walikua katika majaribio yani kabla camera aijawashwa lazma Muongozaji aone mnachofanya kma iko sawa ndo camera inawashwa sasa ktka majarbio haya kuna watu pemben na mambo ya insta ndo watu wanapost kwamba wapo location sasa unapopost bila kujua nakuponda au kushangaa mnakua mnazingua mjue kwanza ndo mpost ..sjui tumeelewana wajameni!!?”
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment