Hivi ni mimi tuu bado niku nyuma ama ndo kuamka kwa tamaduni zetu za kiafrika? Siku hizi bwana mambo yame kuwa moto moto baina watoto wa kike na mapenzi.
 Nilikuwa naangalia video clip moja iliyosambaa sana kuhusu representative wa Tanzania kwenye Big Brother Africa na kijana wa kiganda nikasema kweli eh, kazi ipo, maadili yamekwishaaaa.


Well, I guess kwa kiasi fulani hakuna wa kulaumiwa ila sisi wenyewe watanzania kama washabiki wa reality TV.  Wasio na mfupa wa aibu ndo hao hawaoni tabu kufanya mavituz wazi wazi na kuachia wenye macho wa enjoy LOL. Anyways, kuiga kutatushinda....ninayotaka kuyaongelea leo yanaendana kidogo na ya hapo juu.

Kama mama, je unamwaandaaje mtoto wa kike katika kuyajua maisha ya mapenzi? Sijui kama mila zimebadilika au la, lakini najua mambo yamebadilika kidogo sikuhizi, ukizingatia na tulikotoka.

 Zamani ilikuwa ni mwiko kuongelea mambo ya mapenzi, iwe na wazazi au namarafiki zako, ikisadikiwa kwamba haikuwa tabia nzuri.
 Yaani ilikuwa ni mwiko! Kitu cha kushangaza ni kwamba wazazi wengi hawakuwa wanaelezea kwa undani, ni kwanini si vizuri kuongelea mambo ya mapenzi wazi. Well, sijui ni kwamba wazazi wengi walikuwa in denial kwamba watoto wao hawatakuwa siku moja au vipi? Halafu sasa walikuwa wanasahau kwamba, kuwa mtoto ni ushujaa wa kuwa curious. Haswa unapokatazwa kufanya kitu fulani ndo kama vile umeambia the opposite yaani kwamba "nenda kafanye ulichokatazwa" lol.
 Hata ilikuwa kwamba ukiwa darasani wakati wa kipindi cha biolojia, unamwona mwalimu kabisa akiona noma as well as wanafunzi kuelezea na kusikiliza kuhusu kazi za viungo fulani fulani vya binadamu. 

Matokeo yake sasa, watoto wengi wa kike wamekuwa wakiwa wakubwa halafu very naive-(washamba/wako nyuma) kuelewa developments za maiili yao wenyewe hivyo kujikuta matatizoni. Pia zamani, mara nyingi ulikuwa unaelezwa kwamba mtoto wa kike hatakiwi kuwa karibu na baba yake ama kuvaa nguo fupi ama zinazochora mwili kama anajua atapita mbele ya wanaume. 
Sababu kubwa ya mikanyo hiyo ilikuwa ni kwamba; eti wanaume ni wepesi kufadhaika na ni rahisi sana kumbaka msichana kama kavaa nguo zilizo chora sana. Sikatai kuhusu mifadhaiko but does that mean wanawake ndo hawanaga mifadhaiko au? Well, in the case ya kuvaa nguo za kuchora wateva, hivyo inamaanisha hata wamama waliokuwa wakitoa mikanyo sana kuhusu kutokuwa karibu na madingi, does that mean walikuwa wanaogopa baba mtu anaweza kubaka mtoto wake mwenyewe?? Well, for me, That's just straight up crazy and kuna ukasoro fulani katika akili if thats the case.

Hivyo kutokana na kwamba watoto wengi wa kike wanakuwa- bila- kuwa karibu na baba zao, wengi wao kutoka umri mdogo wanaishia kupaparika wakitafuta attention kutoka kwa wanaume ama unakuta wanakuwa attracted so fast and so much kwa wanaume haswa wanapokunduwa kwamba mwanaume anamfukuzia. Hii ni kwasababu mara nyingi, unakuta wamemiss ama wamekosa some sort of male figure attention kutoka hukoooo majumbani mwao. 
Pia saa nyingine unakuta kuna mambo fulani fulani ambayo mtu angependa kuyaongelea na mama yake lakini since mama ndo mkali/mchungu kama mbogo basi hawezi, na hata hivyo, siku zote msichana huyo amekuwa akijua kwamba majukumu yake kama msichana ni kujua jinsi ya kurun  nyumba mama asipokwepo.
 Hivyo basi msichana anapopata mtu wa nje ambaye anaweza kuongea nae kitu chochote from kuwa na menstrual periods mpaka madukuduku mengine yaliyojaa moyoni na akasikilizwa na kupewa feedback flani, basi we ndo hapo hapo mambo yanapoanza. Wasichana wengi wanaend up kurely sana emotionally kwa mtu huyo (rafiki) ambaye mara nyingi huwa ni rafiki wa kiume. Ukumbuke huyu rafiki wa kiume anaplay role ya kama kaka (kupiga stori), kama baba (kutoa ushauri) na kama rafiki wa karibu sana.

Kitu kikubwa nadhani wamama saa nyingine wanapokosea katika malezi ni kuto kumwelimisha mtoto wa kike kuhusu KUPENDA na KUPENDWA. Pia wanasahau kuelimisha watoto wa kike kuhusu ndoa, na jinsi kwamba kama mtoto wa kike, ni vizuri kujua kujituma ukiwa ndani ya nyumba na pia ni vizuri kujua jinsi ya kujiexpress mahitaji yako na jinsi unavyojisikia moyoni.

 I think wamama wengi especially wa kiafrika wameshazoea kuhenyeka na kunyanyaswa na wanaume eidha wame zao ama wanaume tuu kwa ujumla basi hata hawajui tena wao wenyewe wana deserve kutritiwa vipi na kuheshimiwa vipi na wanaume. So wanatake kipigo tuu kwasababu "MWANAMKE LAZIMA UWE MVUMILIVU."

Pia the notion kwamba mwanamke elimu, ijapokuwa sikatai kwamba ni notion nzuri, nadhani pia elimu bila kujitambua mwenyewe haitasaidia. Ndo maana unakuta mwanamke anaweza kuwa na elimu, hata na  kazi yake nzuri tuu lakini yuko bado anahenyeka na kudhalilishwa na mwanaume kwasababu hana enough courage ya kusimama na kujiuliza nini kinachomata kwenye maisha yake, besides mwanaume. 
Nadhani, kama akina mama ili kuweza kuwaandaa watoto wetu wa kike vyema kwa ajili ya haya maisha, ni muhimu zaidi kumwelimisha msichana kuhusu kujitambua nafsi yake kwanza, kujiheshimu of coarse, kujua kazi za ndani kama mwanamke, kujielimisha kishule na kujua nini maana ya kupenda na kupendwa. Hapo ndipo tutakuwa TUMEMWOKOA MWANAMKE KATIKA JAMII.

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top