Askari wa jeshi la polisi wakiwa eneo la hospitali ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita |
Mwili wa marehemu ukiwa umewekwa sakafuni/kwenye korido kutokana na hospitali ya wilaya ya Mbogwe kukosa mochwari |
Jeshi
la polisi wilayani Mbogwe mkoani Geita linashikilia mwalimu wa shule ya
msingi Kasandalala wilayani humo Laideth Constantine mwenye umri wa
miaka 33 baada ya kumnyonga mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka 7 akiwa
kwenye nyumba ya kulala wageni(Gesti).
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo
kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa geita Joseph Konyo amesema tayari
wanamshikilia mtuhumiwa baada ya vipimo vya daktari kudhibitisha kuwa
mtoto huyo kanyongwa.
Baadhi
ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwalimu huyo amekuwa na mambo ya
kushangaza jamii kwani wakati mwingine anajifanya mlokole,mara anakuwa
mkali na kugombana na kila mtu hasa wakati akiwa shuleni.
“Tumekuwa
tukimshangaa mwalimu huyu,kuna wakati anakuwa mlokole,wakati mwingine
anakuwa,mtaratibu sana,sisi tunashangaa sana kutokea kwa tukio
hili”,walisema.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita
Cosmas Kilosa amesema vipimo vinaonesha kuwa mtoto huyo amefariki dunia
kwa kunyongwa.
Na Philip Chimi-Mbogwe
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment