NI Jumatano tena, safu hii bado inahusika katika kuwaleteeni mambo mazuri ikiwa ni njia ya kuelekea kwenye elimu ya maisha ya uhusiano wa wawili.Baada ya wiki iliyopita kumalizia mada ya Mwanamke akiolewa, kuna ulazima wa kutumia jina la ukoo wa mumewe? Leo tunaanza mada nyingine. 
 
Mada yetu ya leo ni UNAMWACHA, UNAMDAI KILA ULICHOMNUNULIA! Ni mada yenye mapana kwa maana ya wawili wapendao, walioitana ‘honey’ sweet’, baby, mpenzi, darling, mahabuba, laazizi na majina mengine lakini yenye kuonesha kwamba wawili wanapendana kwa dhati. 

Imekuwa ikidaiwa kuwa, licha ya kuitana kwa majina hayo mazuri, baadhi ya wapenzi, hasa wanaume wamekuwa wakidai vitu walivyowanunulia wapenzi wao hao kwa sababu eti wameachana!
Kabla ya kuandika mada hii, wiki iliyopita nilibahatika kuzungumza na wadau mbalimbali ambapo wengi walithibitisha kutokea kwa hali hiyo kama si kwa kusikia, kwa kuona kwa watu wao wa karibu au kuwapata wao wenyewe. 

WASEMAVYO WANAWAKE
Yvonne, mkazi wa Kigogo ya Ruhanga jijini Dar es Salaam, yeye alisema aliwahi kukutwa na tukio hilo miaka mitatu iliyopita. 

lisema: “Nilishangaa sana. Aliniacha mwenyewe lakini cha ajabu akasema nimrudishie vitu vyake vyote alivyoninunulia wakati wa kupendana kwetu.“Alichukua kila kitu, alifika hatua akadai hata ‘kufuli’ zake mbili. Alisema alitaka mwanaume atakayekuwa na mimi baadaye aanze upya.” 
 
Furaha, mkazi wa Mikocheni yeye alisema aliwahi kuachwa na mwanaume baada ya kumfumania. Lakini alipoachika, mwanaume wake akamnyang’anya kila alichomnunulia kwa pesa yake. 



“Nilimuuliza nimekufumania wewe, umeniacha wewe, unadai vitu vyako wewe, ni haki kweli? Akasema vitu vyake lazima achukue kwa sababu alitoa pesa aliyoipata kwa jasho lake. 

UMAKINI NA VITU VYA WANAUME HAWA
Malalamiko mengi ni ya wanaume kuwanyang’anya wake zao au wapenzi wao vitu walivyowanunulia. Nachelewa kwamba, hali hii imekuwa kero kwa wanawake wakiamini ni udhalilishaji. 

Wengi wa wanawake wanasema kuwa, mapenzi ya sasa hata mwanaume akikununulia gari kuwa nalo makini kwani wengi wanaweza kukupa kadi feki, siku akikumwaga anachukua gari lake kiulaini kabisa.

Itaendelea wiki ijayo.

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top