Irene Neema Vedastous 'La Veda'.
Stori: Gabriel Ng’osha
MWANADADA aliyewakilisha Tanzania katika shindano la BIG BROTHER 2014 ‘HOTSHOTS’ nchini Afrika Kusini. Irene Neema Vedastous 'La Veda' ameitwa tena ili kushuhudia fainali za kinyang’anyiro hicho.
Mrembo huyo amepanda pipa juzi saa 8 mchana kuelekea Sauz ambapo atakaa kwa muda wa wiki moja.

Akizungumza na mwandishi wa tovuti hii, La Veda alisema ameitwa Sauz japo bado hajajua anaenda kufanya nini hasa japo anaamini hataingia kwenye jumba la BBA kama mshiriki.
‘’Nimeitwa BBA ila si kwa maana ya kushiriki bali kama mmoja wa washiriki ili kushuhudia fainali za BBA zinazotegemea kufanyika hivi karibuni.
Ninafurahi kwa sababu nitakutana na washiriki wenzangu, kama nikibahatika kupata nafasi ya kuimba, wimbo wangu mpya wa LET IT GO, nitafanya makubwa sana maana muda mwingi na akili yangu nimeviwekeza kwenye muziki, nitakuwa Sauz kwa wiki moja kisha nitarejea nyumbani kujipanga zaidi kimuziki" Alisema La Veda.
Aidha La Veda amemtakia kila la heri mshiriki mwenzie Idris Sultan ashinde na amewaomba Watanzania kumuombea kwani ushindi wake ni ushindi wa Watanzania wote.

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top