Nyemo Chilongani MADAI!
Mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Severin Daniel Ndauka
amejitokeza katika Ofisi za Global Publishers na kudai kwamba, staa wa
sinema za Bongo, Rose Donatus Ndauka ni mtoto wa kaka yake ambaye
alichukuliwa kutoka Tanga na kupelekwa jijini Dar.
Mzee huyo aliyekuwa akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi
wetu, alisema mwaka 1979, shemeji yake, Nyazimbili au mama Godwin
(anayedaiwa ni mama wa Rose) alijifungua mtoto wa kike katika Kijiji cha
Sakura wilayani Pangani, Tanga ambapo kwa bahati mbaya mama huyo
alifariki dunia hivyo mtoto kuchukuliwa na kanisa ambalo lipo Msimbazi
Dar hakutaka kulitaja jina lililomlea mtoto huyo kwa kuwa familia
haikuwa na uwezo.
“Baada ya hapo, hatupata taarifa tena lakini mimi niliamua kuja Dar
kwa ajili ya kumtafuta Rose. Nilikwenda Msimbazi, nilipofika nikaambiwa
Rose alichukuliwa na kituo cha kulea watoto kilichopo Kurasini. Ilibidi
niende Kurasini, kufika nikaambiwa alichukuliwa na msamaria mwema kwa
ajili ya kumlea kama mtoto wake.
Staa wa sinema za Bongo, Rose Donatus Ndauka.
“Tangu hapo hatukupata taarifa nyingine lakini baadaye dada yangu
anaitwa Maria Ndauka akanipigia simu, akasema amemuona Rose kwenye
televisheni akiigiza na marehemu Steven Kanumba ndiyo nimekuja hapa
mnisaidie kumpata,” alisema mzee huyo.
Rose alipotafutwa na kuelezwa ishu hiyo, alisema alizaliwa jijini Dar
na si mwaka 79 kama alivyodai mtu huyo na kwamba katika Kijiji cha
Sakura hana ndugu.
Kama kuna Rose Ndauka mwingine, afike Ofisi za Global Publishers
zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar ili akutanishwe na mzee huyo.
Mhariri.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment