Hata
kwa wanawake nao huwa wanaangalia wanaume ‘handsome’ ambao hata wakiwa
wanatembea pamoja mtaani watavuta macho ya watu na kusifiwa.
Mimi sidhani kama wanaoangalia vigezo hivyo wanakosea hasa kama
wanatafuta wapenzi na wachumba watakaotengeneza njia ya kuelekea kwenye
ndoa.
Naomba katika hili nieleweke kwamba, suala la muonekano wa mtu si
kigezo tosha cha kumruhusu awe sehemu yako katika maisha ya ndoa. Wapo
ambao ni ‘handsome’ na warembo lakini kiukweli hawastahili kupewa nafasi
ya kuingia nao kwenye ndoa.
Tatizo la wanaume ‘handsome’
Utafiti nilioufanya ambao siyo rasmi unaonesha kwamba, ni wachache sana waliooa wanawake wazuri na wakaishi muda mrefu tena kwa furaha na amani.
Utafiti nilioufanya ambao siyo rasmi unaonesha kwamba, ni wachache sana waliooa wanawake wazuri na wakaishi muda mrefu tena kwa furaha na amani.
Tunachotakiwa kujua katika hili ni kwamba, kuna baadhi ya wanaume
ambao wanajijua wanapendwa sana na wanawake kutokana na muonekano wao.
Kwamba ni warefu, ni watu wa mazoezi, wana sura nzuri na sifa
nyinginezo.
Wenye sifa hizi ni chaguo la wanawake wengi. Kutokana na hilo sasa,
wapo ambao wana kaulimbukeni f’lani ka’ kushindwa kutulia na mwanamke
mmoja. Wanaweza kuingia kwenye ndoa lakini bado wakashawishika kutembea
na wanawake wengine kwa kuahidiwa fedha na vitu vingine.Mbaya
zaidi, wanaume wa dizaini hii watakuwa wanajisahau kwamba nyumbani wana
wake zao ambao wamewakabidhi mioyo yao na hawatarajii kusalitiwa.Hapo
ndipo tatizo litakapoanzia na kumfanya hata mke mwenyewe ajute kuingia
kwenye ndoa na mwanaume ‘handsome’. Sisemi kwamba wanaume ‘handsome’
wote ni tatizo kwenye ndoa, la hasha!
Wapo ambao ni watulivu, wasio viruka njia, kwamba wakipenda mmoja
wamependa na hata wakishawishiwa na wengine, husimamia hisia zao na
kuangalia heshima yao mbele ya jamii.
Tatizo ni kwamba, kuna ambao kwa muonekano huwezi kuwajua lakini ukishakubali ndoa utashangaa usumbufu utakaopata.
Tatizo ni kwamba, kuna ambao kwa muonekano huwezi kuwajua lakini ukishakubali ndoa utashangaa usumbufu utakaopata.
Utaona mumeo ana marafiki wengi wa kike na ukimuuliza anasema ni
marafiki tu. Mara utamuona anabadilisha magari na ukifuatilia utaambiwa
ni magari ya mwanamke f’lani mwenye nazo. Hapo sasa ndipo utajua kwamba
kumbe hujapenda peke yako, wapo wengine waliopenda na wakapewa nafasi
kutokana na ushawishi wao.
Ndiyo maana nasema kuolewa na mwanaume ‘handsome’ tena ambaye ni
limbukeni, utapata tabu sana. Utaambulia ile sifa tu ya kwamba umeolewa
na mwanaume mzuri lakini kumbe hafai kuitwa mume!
Wasichana warembo nao!
Jaribu kuchunguza utabaini kuwa, asilimia kubwa ya wanaume wanaoteswa na ndoa zao, wameoa wasichana warembo lakini wasiojua thamani ya ndoa. Watakuwa wanaona sifa kuolewa lakini bado hawajui namna ya kuzitunza ndoa zao.
Jaribu kuchunguza utabaini kuwa, asilimia kubwa ya wanaume wanaoteswa na ndoa zao, wameoa wasichana warembo lakini wasiojua thamani ya ndoa. Watakuwa wanaona sifa kuolewa lakini bado hawajui namna ya kuzitunza ndoa zao.
Watakuwa warahisi kushawishiwa na wanaume wakware na wakati mwingine
wakiona wanatongozwa sana kutokana na uzuri wao, wanavimba
vichwa.Wanakuwa si watulivu kwenye ndoa zao, siyo watiifu kwa waume zao
na wanafanya hivyo wakiamini kwamba hata wakiachika, watapata wanaume
wengine wa kuwaoa.
Ndiyo maana huwa nasema mara kwa mara kwamba, ukitaka kuoa ni lazima
uangalie mwanamke mzuri unayemuona wewe. Lakini usiishie hapo, angalia
na tabia zake ili usije ukaingia kwa mtu ambaye hawezi kukupa furaha ya
ndoa uliyotarajia.
Katika hili naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, ukitaka kuingia
kwenye ndoa epuka sana kuangalia muonekano wa mtu. Tukijichanganya macho
yatatuingiza mkenge!Unaweza kumuona msichana mzuri, mwenye figa na sura
ya kuvutia au mwanaume ‘handsome’, mwenye sifa zote za kupendwa na kila
mwanamke lakini kumbe linapokuja suala la ndoa, hamna kitu!
Ni suala la wewe kuwa makini sana hasa pale unapotafuta mpenzi au
mchumba! Achana na ile tabia ya kutafuta sifa kwamba eti ‘kapo’ yenu
inavutia, swali ni je, anaiheshimu ndoa na siyo macho juujuu?
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment