Siku chache baada ya kumwagwa na Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’, Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amenaswa kwenye mahaba mazito na msanii, mtangazaji, mjasiriamali, tajiri na mrembo mkali kuliko wote Afrika Mashariki,  Zarinah Hassan a.k.a Zari au Boss Lady.

Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akimhagi msanii mrembo mkali kuliko wote Afrika Mashariki,  Zarinah Hassan a.k.a Zari au Boss Lady.

HABARI YA TAUNI
Habari ya ‘mujini’ ilidai kwamba, mahaba ya wawili hao yalianzia safarini walipokutana kwenye ndege moja wiki iliyopita ambapo Diamond alikuwa akitokea nchini Nigeria kupitia Afrika Kusini kisha Dar huku Zari akitokea Afrika Kusini kuelekea Dar kibiashara.


Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa hao walipokutana kwenye ndege waliungana na kupiga picha za pamoja kisha safari yao ya mahaba niue ikaanzia hapo

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top